Kenya yaitaka Uingereza iwachukulie hatua polisi wake 'waliomtesa Mkenya'

Kenya yaitaka Uingereza iwachukulie hatua polisi wake 'waliomtesa Mkenya'

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
1602588817915.gif

Kenya imeiandikia Uingereza ikidai haki juu ya ukatili dhidi ya raia wa Kenya unaodaiwa kufanywa na maafisa wa polisi katika eneo la Colchester, Essex nchini humo.

Tukio la ukatili huo lilichukuliwa kwenye picha ya video ambayo ilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii na kuibua hasira na vilevile kuchochea vugu vugu la ‘Black Lives Matter’ dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Katika video hiyo, polisi takriban sita wa Uingereza wanaonekana wakimtesa Mkenya aliyetambuliwa kama Wycliff Cox walipokuwa wakitaka kumkamata kwa madai ya kukiuka sheria za dhamana.

Maafisa hao wanaonekana wakikandamiza kichwa cha Wycliff ardhini huku wakishikia shingo yake, huku watu wa familia yake ikitazama na mama yake akisikika akiomba : “Usimuue kijana wangu.”

Huku uso wake ukionekana kutoka damu, mikono na miguu ikiwa imefungwa, Wycliff, ambaye ameripotiwa kuwana ugonjwa wa akili, anaonekana akichukuliwa na polisi na kuingizwa ndani ya gari la polisi lililokuwa linasubiri.

Katika taarifa yake iliyotolewa Jumatatu , Ubalozi wa Kenya nchini Uingereza ulitoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua dhidi ya mafisa hao kwa ‘’matumizi ya nguvu zisizo za lazima kwa mtu ambaye hakuwa na silaha.

“Ubalozi wa Kenya nchini Uingereza umepokea video ya kusikitisha inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ambapo polisi katika Colchester, Essex wanaonekana wakimtesa Mkenya , Bw. Wycliff Cox,” alieleza taarifa ya ubalozi wa Kenya nchini Uingereza:
 
Wao si ndo wanajipendekezaga Kwa Wazungu,hata raisi wao anaendaga huko kuomba msaada wacha wawavurugee.

Hapa Bongo namkubali Sana babangu Mzee Magu hajawahi kukanyaga kwao hata siku moja.

Wao wenyeweee fika hawawezi kuishi maisha yao bila kutegemea Africa.

Sa nashangaa tunawashobokea.

Ila Kwa hapa Bongo natamani tuu wale walio kuwa wakoloni eti waje tena wazuge wanataka kututawala ndo watajua kuwa

Kumbe kuna watu wanaweza mkata kata Mzungu na kumuinjika Jikon akaiva akaliwa na pili na ugali.

Kwakuwa sijawahi kuwapenda wale binadamu hata kidogoo.

Maana ndio wameleta mauji sanaaaa
Rwanda 1994 Kombati

Na mwengineko.

Kweli wanatuumiza Sanaa hatujui tuu.
 
Polisi wa Afrika wakoje? Huwa wanaact vipi kwenye scenario kama hiyo?
 
Wao si ndo wanajipendekezaga Kwa Wazungu,hata raisi wao anaendaga huko kuomba msaada wacha wawavurugee.

Hapa Bongo namkubali Sana babangu Mzee Magu hajawahi kukanyaga kwao hata siku moja.

Wao wenyeweee fika hawawezi kuishi maisha yao bila kutegemea Africa.

Sa nashangaa tunawashobokea.

Ila Kwa hapa Bongo natamani tuu wale walio kuwa wakoloni eti waje tena wazuge wanataka kututawala ndo watajua kuwa

Kumbe kuna watu wanaweza mkata kata Mzungu na kumuinjika Jikon akaiva akaliwa na pili na ugali.

Kwakuwa sijawahi kuwapenda wale binadamu hata kidogoo.

Maana ndio wameleta mauji sanaaaa
Rwanda 1994 Kombati

Na mwengineko.

Kweli wanatuumiza Sanaa hatujui tuu.
Iyo mitumba uliyovaa apo umetengeneza wewe???[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Iyo mitumba uliyovaa apo umetengeneza wewe???[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Kwani kabla hawa wasengerema wenzio hawaja leta taka taka zao we ambae unazihusudu.Sisi tulikuwa na mavazi yetu ya Ngozi za wanyama na maskio ya tembo
Tulikuwa na tamaduni zetu na wake zetu tukifaidi ndoa za mitala ambapo sasa imekuwa shida.

Tulikuwa na burudani zetu za ngoma tukikesha na Miungu yetu kabla hawa jamaa na Sera zao za mashoga wenzako.

Kweli tulifurahia maisha yetu.
Ila kwakuwa wewe umeona mitumba ndo maisha kwako vyemaaaa sanaaa
 
Back
Top Bottom