Kenya imeonyesha matumaini makubwa ya kupewa nafasi ya kuandaa sherehe za ufunguzi na kufunga mashindano ya AFCON 2027, yatakayoandaliwa kwa pamoja na Kenya, Uganda na Tanzania.
Local Organising Committee (LOC), inayoongozwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CECAFA Nicholas Musonye, imewaambia wabunge kuwa maandalizi ya Kenya yamefikia takriban asilimia 80.
Kadi kubwa ambayo Kenya inaweka mezani ni Talanta Raila Odinga Stadium. Musonye amesema ujenzi wa uwanja huo umefikia takriban asilimia 95, hali ambayo anaamini inaipa Kenya nafasi nzuri ya kuchaguliwa kuandaa matukio hayo mawili muhimu.
Akizungumza mbele ya Kamati Teule ya Bunge kuhusu Regional Integration, Musonye alisema pia Kenya ina faida kutokana na uwezo wake wa usalama na hospitality, mambo ambayo yatakuwa muhimu wakati CAF itakapofanya tathmini ya maandalizi ya wenyeji.
AFCON 2027 inatarajiwa kufanyika kati ya Juni na Julai 2027, ikiwa ni mara ya kwanza kwa Kenya, Uganda na Tanzania kuandaa kwa pamoja mashindano hayo makubwa zaidi ya soka barani Afrika.
Hata hivyo, kauli ya LOC bado si uthibitisho wa mwisho kwamba Kenya imepewa ufunguzi na fainali. Kinachosisitizwa kwa sasa ni kwamba nchi inaamini ina nafasi kubwa ya kupata heshima hiyo kutokana na maendeleo ya maandalizi yake.
Baada ya East Africa kuonyesha uwezo wake kupitia CHAN, sasa macho yanaelekezwa kwenye jukwaa kubwa zaidi la soka la Afrika.