Kenya yakataa wito kutaka Marekani isuluhishe mgogoro

Kenya yakataa wito kutaka Marekani isuluhishe mgogoro

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje, Macharia Kamau amesema hakuna haja ya mazungumzo kwa kuwa Kenya imefanikiwa kupitia mzunguko wa uchaguzi wa miaka mitano na sasa inazingatia kuwahudumia raia wake.

PIC+KENYANWITO.jpg

Serikali imekataa wito unaotaka Marekani iingilie kati mgogoro wa sasa wa kisiasa dhidi ya upinzani.
Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje, Macharia Kamau amesema hakuna haja ya mazungumzo kwa kuwa Kenya imefanikiwa kupitia mzunguko wa uchaguzi wa miaka mitano na sasa inazingatia kuwahudumia raia wake.
Kamau alikuwa akijibu makala iliyochapishwa mwishoni mwa mwezi uliopita na mabalozi wa zamani wa Marekani nchini Kenya Johnnie Carson na Mark Bellamy ambao walitaka Marekani iingilie kati hali ya Kenya.
"Jibu letu kwa ombi la kipuuzi la waandishi kutaka uingiliaji wa Marekani nchini Kenya kwa sauti kubwa ni hapana, shukrani," amesema katika taarifa Jumanne.
"Hiki ni kielelezo cha wazi cha jinsi mawazo yaliyotangulia na yaleyale juu ya Afrika kutoka kwa wataalamu hawa wa nchi za Magharibi wanavyoathiri uzoefu wowote na maarifa ambayo wanaweza wawe wameyapata katika bara. Weledi wao wa kukosea juu ya masuala ya Kiafrika na ya Kenya siyo tu unashangaza bali pia unaonyesha kwa nini tafiti zinazofanywa kwenye madawati juu ya Afrika, na chanzo pekee cha habari kikiwa kile kinapendelea vyombo vya habari vya Magharibi, unapaswa kushughulikiwa kikamilifu kwa kukataa," amesema.
Msemaji wa Rais Uhuru Kenyatta Manoah Esipisu alionekana kuthibitisha kuwa, kwa kweli, huo ndio msimamo alionao Mkuu wa Nchi.
"Katibu Mkuu amesema na huo ndiyo msimamo. Je, unataka kuongeza nini?" ameuliza.

Chanzo: Mwananchi
 
Kuna Msemo Unasema " Usitanue Msuli Kama Upaja Wako Mdogo "
Hao jamaa hawawezi kupanua msuli kwa mzungu, Hapo ana jibu report ya kwenye gazeti ambayo mwandishi alihoji mabalozi wastaafu. Kama ingekua wamelimwa barua kutoka white house vingekua vidogo kama kifaranga kilicho mwagiwa maji.
 
Aisee, umenikumbusha Tz mlivobadilisha gia angani, kuhusu ile marufuku yenu ya mitumba. Wala hakuna barua yeyote ile mliyoipata kutoka kwa POTUS. Ndio yale ya mbwa koko na mkia wake katikati ya miguu.
 
Aisee, umenikumbusha Tz mlivobadilisha gia angani, kuhusu ile marufuku yenu ya mitumba. Wala hakuna barua yeyote ile mliyoipata kutoka POTUS. Ndio yale ya mbwa koko na mkia wake katikati ya miguu.
Issue ya mitumba hujaielewa, bado hakuna officially agreement, wameprolong the negotiations, still figuring out the way, because so much is at stake here, ondoa kabisa wamarekani kwenye equation, so much is at stake to the wananchi, and that is what matters, kunazo njia kibao za kudiscourage hiyo kitu. Usichekelee, bado mpira upo dimbani.
 
Hii comment yako ina kauvundo ka kijasho chembamba. Waoga nyie, yaani sasa hivi mnavaa mitumba kwa shuruti ya Donald Drunk. Marufuku ilikuwa kwenye akili zenu tu.
 
Back
Top Bottom