Kenya yaomba msaada wa chakula tani 200,000 za mahindi kutoka Tanzania

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,575
Kenya imeomba msaada wa chakula kutoka Tanzania kiasi cha tani laki mbili (200,000t).Tanzania imekubali na makubaliano yameishasainiwa jana nchini Kenya baina ya waziri wa kilimo chini ya balozi wa Tanzania.

Wafanyabisashara wa kitanzania watasafirisha na kuuza mahindi nchini Kenya kutoka maghala ya taifa Arusha na DSM.Gunia moja kilo 90 litauzwa shilingi 2650 (2650X19tsh) za Kenya na kusafirisha ni sh.300 za Kenya.

Tanzania imeagiza Kenya zoezi kuanza mara moja


Kilimo kwanza oyee.

 
Vibali vinatolewa vp au hakuna vibali?? Maana kwenye vibali ndio inakuaga urasimu
 
Huu ndiyo uimara wa uchumi katika Serikali ya CCM.
 
vibali vitatoka kwa rushwa
_chezea wazee wa takrima we!
 

Hivi hoja hapa ni Kenya kuomba msaada wa chakula au Kenya kuomba kununua chakula kutoka Tanzania?
 
Tanzania wange safirisha unga badala ya mahindi.Tukoje Tanzania!
Pia tungesafirisha mazao mengine yatokanayo na mahindi kama pumba n.k
Maghala ya NMC na mashine zake tumewapa wawekezaji feki,kwa bei ya kutupa yanachakaa bila kutumika.
 
Huu ndiyo uimara wa uchumi katika Serikali ya CCM.
Mahindi niliyolima kwa gharama zangu yanauhusiano gani na serikali ya CCM. Tangu nianze kilimo hajawahi fika hata mjumbe wa nyumba kumi wa CCM shambani kwangu iweje uhusishe mahindi ya watu na CCM
 
Mahindi niliyolima kwa gharama zangu yanauhusiano gani na serikali ya CCM. Tangu nianze kilimo hajawahi fika hata mjumbe wa nyumba kumi wa CCM shambani kwangu iweje uhusishe mahindi ya watu na CCM

Wacha uongo wewe.
 
Tanzania wange safirisha unga badala ya mahindi.Tukoje Tanzania!
Pia tungesafirisha mazao mengine yatokanayo na mahindi kama pumba n.k
Maghala ya NMC na mashine zake tumewapa wawekezaji feki,kwa bei ya kutupa yanachakaa bila kutumika.

Hao unaowaita wawekezaji feki Bakhresa ndiye msambazaji wa kwanza wa unga wa ngano Afrika Mashariki na ya kati, na hizo mashine zote za kizamani kaondoa, sasa hivi watu wana "bofya" tu.

Uko wapi, umelala?
 
mahindi niliyolima kwa gharama zangu yanauhusiano gani na serikali ya ccm. Tangu nianze kilimo hajawahi fika hata mjumbe wa nyumba kumi wa ccm shambani kwangu iweje uhusishe mahindi ya watu na ccm

kilimo kwanza; ruzuku ya pembejeo na mbegu bure

sera ya ccm, chezea ccm wewe utajuta kuwafahamu 2015. Tutlisha na south sudan na somalia .
Giant of economy inakuja
 
Nyinyi watu hamna pema,paku pongeza pongezeni.ruzuku zote hata Ofisi moja hamjajenga.

Ofisi ni muhimu saa mkuu KWELI!, ila ukumbuke kwamba Kuwa na ofisi zenye viwango vya ubilionea si kigezo cha utendaji na ufanisi bora wa kazi. Mfano mzuri ni CCM na miiko aliyokuwa akilia nayo Nyerere!
 
Ni vyema tukawa bega kwa bega na jirani zetu wakati wa shida na furaha. Ikiwa sisi tutakula na kushiba na jirani zetu wana njaa, sisi ndio tutabeba mzigo wa dhambi. Huu ni wajibu wetu wa mwanzo na huu si msaada ni lazima kwetu, hatuwezi kushiba wakati wenzatu wanalala na njaa.

Tena kama hawana fedha hata bure tutawapa jirani zetu.

Ahsante Jakaya kwa kuona mbali, kuja na ubunifu wa hifadhi ya chakula na kilimo kwanza.
 
Watani wetu wananjaa sana Tanzania ikiweka ngumu wakenya watakufa kuliko waethiopia walivyokufa miaka 80s.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…