Kenya yaomba msaada wa chakula tani 200,000 za mahindi kutoka Tanzania

Kenya yaomba msaada wa chakula tani 200,000 za mahindi kutoka Tanzania

Ujinga wa watanzania ndio uko hapo, badala ya watu kuona hii kama fursa ya kufanya biashara wanaona kama wanatoa msaada na kujivuna. Huu ni uchanga katika biashara. By the way ilitakiwa kuwa na free movement of goods bila hata kuomba vibali ili mkulima wa Tanganyika anufaike na soko la Kenya na popote pale. Huu uzembe wa kutotambua fursa umeletwa na CCM

Wengi wameshiba propaganda hawawezi kupambanua jema lipi baya lipi. Hii ni fursa ya kuchangamkia hasa biashara ya mchele.
 
Nashangaa sana. Nilidhani hii ingekuwa mada yenye kufungua akili zetu, naona imeishia kukejeli na kudhihaki, yale yale ya Simba na Yanga.

Kenya kununu chakula Tanzania ni jambo zuri sana. Hii ndilo akina Nyerere na wenzake walikaa katika south south commission na kulijadili. Kwamba, tuanze kushirikiana wenyewe kwanza kabla ya kukimbilia Washington kwa IMF ambaye siku zote hutoa damu kwa kutumia riba na masharti.

Sijaona tatizo lolote zaidi ya faida kwa nchi zote mbili kuanza biashara za maana kama hizi.
Kesho tutawaomba jambo jingine badala ya kwenda Brazi au China.

Pili, kwa Watanzania nilidhani hili lingekuwa la kufungua macho na akili zetu.
Kumbe tuna uwezo wa kuuza tani 200,000 Kenya!!!

Basi tunaweza kuwa na uwezo wa kuuza tani milioni 100 kwa Malawi, Zambia, Uganda, Rwanda na Burundi.
Hilo tu linaweza kutufanya tuwe power house ya EAC.

Tulichotakiwa ni kuchukua jambo hili na kujiuliza, tufanyeje? Ardhi ipo ya kutosha, watu tunao na soko ndio kama hilo linatuhitaji wala si kuwa tunatafuta. Wapi tumekwama na kwanini. Haya ndiyo maswali ya kujiuliza.

Tatu, kwa upande wa Kenya, nao ni somo zuri kuwa fimbo inayoua nyoka ni ile iliyopo mkononi.
Kwamba, hata kama watakuwa na CoW, je hiyo inatosha katika kukidhi haja zao.
Na je ni busara kukimbia ukiacha milango wazi au ni vema ukaenda kwa utaratibu ukihakikisha usalama wa nyumbani kwako?

Ni hayo tu
 
SUKARI PIA HIPO YA KUTOSHA UNAOZEA KWENYE MAGHALA; TUNAWAKALIBISHA WAJE WANUNUE , MTIBWA ,KAGERA ALOT OF TONNES:bump:
 
kumbe mahindi ya kutosha yapo tz??....sasa kwann msishushe bei kilo ya unga kuwapa wananchi unafuu kidogo wa maisha?
 
sasa hizi ndo fursa za biashara hapa nadhani wafanyabiashara wa Tanzania wangepata faida kubwa sana endapo wangepeleka unga na sio mahindi kwani bei ingepanda kutokana na kwamba uliouzwa ni unga na sio mahindi wangeweza kuwauzia pumba kwa ajili ya mifugo na pia wangewaungisha wajasiriamali wenzetu hapa hapa nyumbani (wenye mashine za kusaga na kukoboa nafaka/ wauza mifuko kwa ajili ya package na kufanya mzunguko wa hela kuwa juu.
 
Basi ndi hawajapata hadi leo...siongeli hewani biashara yangu nafanyia mombasa tunajua ana eneo ila masharti yamemshinda, ndio maana anawauzia diluted syrup necter mnakuywa tu....

Unaota ndoto ya mchana.
 
unamaanisha kuwa wanaume wao wanakunywa sana chang'aa kwa hiyo hawawezi kazi?

Na bado wataomba vingi tu kutoka Tanzania, sisi ndo giant kwa East Afrika kwa kila kitu, walituuo
Ba jet fuel tuliwapa, na wala hawakuomba rwanda wala uganda sababu wote hawachekani, wametuomba chakula tunawapa tena, na bado siku si nyingi watatuomba wanaume wakitanzania tukawaolee dada zao sababu wanaume wakikenya hawajiwezi, Tupo tayari kwa hilo pia, Mi nitakuwa wa kwanza.
 
Basi ndi hawajapata hadi leo...siongeli hewani biashara yangu nafanyia mombasa tunajua ana eneo ila masharti yamemshinda, ndio maana anawauzia diluted syrup necter mnakuywa tu....

hujiulizi kwa nini hakuna product ya bakhresa kenya?
sioni hasa mantiki ya hii michango yako. Ni chuki au nini?
 
Leo wakati wa Kikwete Watanzania mna kauliwa za kutamba na kuwanyanyasa wenzetu kwa mahindi? Mmesahau njaa wakati wa Nyerere mpaka tukawa omba omba wa chakula, tukaletewa unga wa mahindi wa msaada wa rangi ya njano, tukaupachika jina unga wa Yanga. Najuwa wengi wenu ni wadogo na hamkuwepo wakati huo, basi hata hamjahadithiwa? Wacheni kusimanga ndugu zetu wakati wa shida. Kabla ya wazungu kutugawa kwa kututawala tulikuwa sote ni wamoja.

Mmesahau hata Kikwete alivyoipokea hii nchi kutoka kwa Mkapa tulikuwa na njaa? Ndipo Kikwete aka jitahid kuomba misaada na akatutangazia hatokuwa mtu kwa njaa? Na ndipo akaanzisha mpango wa Hifadhi ya chakula?

Tusimsimbulie mtu kwa kupata na majanga, sisi hatujui ya kesho. Haohao tunaowasimbulia leo ndio wanawe za kutusaidia kesho.

Tuwache unazi na ushabiki na ushindani wa kijinga wakati wa majanga. Tuwe bora zaidi ya hivyo.
 
NEW ALERT;~WALE WASHENZI WALIOFANYA MAUAJI MKELETONI KULE MOMBASA WAFANYA MAUAJI MAPYA USIKU HUU WATEKETEZA NYUMBA NA VITUO VYA POLISI POLENI WAKENYA idadi ya vifo bado haija tambulika!
 
kilimo kwanza; ruzuku ya pembejeo na mbegu bure

sera ya ccm, chezea ccm wewe utajuta kuwafahamu 2015. Tutlisha na south sudan na somalia .
Giant of economy inakuja
Mbegu bure??????????
 
Back
Top Bottom