Wakenya wanaelewa maana ya maneno ya katiba yanayosema,
"Wananchi ndiho msingi wa mamlaka, Mamlaka ya Serikali yatatoka kwa wananchi" yaani wananchi ndiyo wenye Serikali na ndiyo wenye mamlaka juu ya Serikali na viongozi wake.
Kwa hiyo kunapotokea wananchi hawataki kitu fulani, Serikali inatathmini kama kweli ni wananchi walio wengi hawataki, au ni kikundi kidogo tu cha wananchi. Serikali ikijiridhisha ndiyo matakwa ya wananchi wengi, lazima serikali itekeleze matakwa ya umma.
Haoa kwetu, wananchi wamegeuzwa kuwa watumwa wa watawala, yaani mtawala akitaka jambo ambalo hata kama wananchi wote hawataki, lazima lifanyike, iwe kwa fimbo, mijeledi, kutekwa au kuuawa. Na wote kwa hofu, baadhi wenye akili ndogo wameamua kujivua akiki na kuwa machawa.