Kenya yashuhudia wimbi la 2 la maambukizi ya Corona Virus kutokana na wagonjwa kuongezeka

Kenya yashuhudia wimbi la 2 la maambukizi ya Corona Virus kutokana na wagonjwa kuongezeka

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Wizara ya Afya humu nchini imeelezea wasi wasi wake kuhusu ongezeko kubwa la idadi ya watu wanaofariki kutokana na ugonjwa wa COVID-19 katika siku za hivi karibuni.

Hii ni baada ya wagonjwa 14 kuthibitishwa kuaga dunia kutokana na makali ya ugonjwa huo, masaa 24 yaliyopita, na kufikisha 964, jumla ya wagonjwa waliofariki humu nchini.

Akitoa taarifa ya kuhusu hali ya maambukizi ya ugonjwa humu nchini kutoka Kaunti ya Mombasa, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema nchi hii inashuhudia wimbi la pili la maambukizi hayo lenye athari zaidi ya lile la kwanza.

“Kama mlivyoona, idadi ya maambukizi, wagonjwa walio hospitalini na wale wanaofariki imeongezeka. Tuko katika wimbi la pili la maambukizi ya virusi hivyo humu nchini,” amesema Kagwe.

Amesema kuwa nchi hii imepoteza jumla ya watu 54 ambao wamefariki kutokana na ugonjwa huo ndani ya juma hili pekee.

Waziri huyo pia ametangaza kwamba watu wengine 761 wamethibitishwa kuambukizwa ugonjwa wa COVID-19 baada ya sampuli 4,830 kupimwa.

Visa hivyo vipya vimeongeza idadi ya jumla ya maambukizi humu nchini hadi 52,612, baada ya wizara hiyo kupima jumla ya sampuli 678,000 tangu virusi hivyo kuripotiwa.

Kagwe amesema kuwa serikali itatoa muelekeo zaidi kuhusiana na hali ilivyo nchini baada ya kikao kilichoitishwa na Rais Uhuru Kenyatta juma lijalo.
 
Kwanini wasikaushe tu hao nao iwe survival of the fittest
 
Pole sana, shida ni kwamba mmeacha kula vyakula vyenu vya asili wengi wa kenya wana jifanya na wao ni wazungu kupenda fast food sanaa mkarango. Kuleni ugali kitu dona., Leguminants plants za kutosha.

Upande wetu corona anaogopa hataaaa kuchungulia
 
Pole sana, shida ni kwamba mmeacha kula vyakula vyenu vya asili wengi wa kenya wana jifanya na wao ni wazungu kupenda fast food sanaa mkarango .... Kuleni ugali kitu dona. Leguminants plants za kutosha.

Upande wetu corona anaogopa hataaaa kuchungulia

Naona wanasiasa wenu wanaikimbia nchi yenu wakija Kenya, huko mumeingiwa na kitu gani hadi mumekua kama wanyama, mlifaulu kufuta upinzani, maandamano yalishindikana, sasa mumeachiwa kutawala bila usumbufu mbona bado mnahangaika kuwasaka na kuwaua wapinzani. Muwaache na kuendeleza uchumi wa nchi yenu.
 
Ah siasa waachie wana siasa wenyewe maana watamalizana wenyewe mimi common mwananchi nadunda na mambo yangu.
 
Ah siasa waachie wana siasa wenyewe maana watamalizana wenyewe mimi common mwananchi nadunda na mambo yangu

Mkiendelea na hayo mauchafu yatawakuta haya, fuata huu Uzi hapa
 
Mkiendelea na hayo mauchafu yatawakuta haya, fuata huu Uzi hapa
Siasa za afrika zote zina tabia moja hata huko kwenu hamna jipya ni yale yale tu ila different cover.

Una weza tazama pale ivory coast. Kinachoendelea. Bagbo alijaribu kumuwekea vikwazo alwatara then alwatara akashinda urais NOW alwatara ana muwekea vikwazo bagbo.
 
Naona wanasiasa wenu wanaikimbia nchi yenu wakija Kenya, huko mumeingiwa na kitu gani hadi mumekua kama wanyama, mlifaulu kufuta upinzani, maandamano yalishindikana, sasa mumeachiwa kutawala bila usumbufu mbona bado mnahangaika kuwasaka na kuwaua wapinzani. Muwaache na kuendeleza uchumi wa nchi yenu.

sasa si mngewapokea!!!kwanini kuwakamata tena na mnajua wanakimbia tabu[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Siasa za afrika zote zina tabia moja hata huko kwenu hamna jipya ni yale yale tu ila different cover.

Una weza tazama pale ivory coast. Kinachoendelea. Bagbo alijaribu kumuwekea vikwazo alwatara then alwatara akashinda urais NOW alwatara ana muwekea vikwazo Bagbo.

Umeona wapi tunaua wanasiasa wetu wa upinzani hadi wanakimbilia ubalozini na wengine kwenda nje ya nchi, ilipaswa aibu iwaingie baada ya kusindika kura zao, sio muendeleze ubabe wa kuwaua.
 
sasa si mngewapokea!!!kwanini kuwakamata tena na mnajua wanakimbia tabu[emoji23][emoji23][emoji23]

Huyo Lema nimemshangaa maana hajatumia akili hapo, alipaswa avae mashuka ya Kimaasai avuke mpaka kimya kimya kisha atinge kwenye ofisi za UNHCR, afahamu mapolisi wa Kenya huwa kimoja na hao wa kwenu, walianza ushirikiano wa pamoja tangu kipindi kile cha magaidi.
 
Pole yao sana majirani. Ila majirani aisee, wanacheza ngoma ya mabeberu.

Cc: mahondaw
 
Umeona wapi tunaua wanasiasa wetu wa upinzani hadi wanakimbilia ubalozini na wengine kwenda nje ya nchi, ilipaswa aibu iwaingie baada ya kusindika kura zao, sio muendeleze ubabe wa kuwaua.
Kipindi cha mzee MoI mlikuwa na AG wenu mmoja alikuwa hatari sanaaa
 
Huyo Lema nimemshangaa maana hajatumia akili hapo, alipaswa avae mashuka ya Kimaasai avuke mpaka kimya kimya kisha atinge kwenye ofisi za UNHCR, afahamu mapolisi wa Kenya huwa kimoja na hao wa kwenu, walianza ushirikiano wa pamoja tangu kipindi kile cha magaidi.
Hao ni wanasiasa wahuni wameshtukiwa.

Haingekuwa sawa, aonekane Kenya akipaka matope nchi, lazima ingetumika nguvu kubwa kumzuia, wameshtuka mapema.
 
Kipindi cha mzee MoI mlikuwa na AG wenu mmoja alikuwa hatari sanaaa

Enzi hizo tuliteseka kama namna Watanzania wanateseka leo, ila tukaamua basi, tukaibuka barabarani kila siku mabomu ya machozi na risasi na maafa, ila tukakomaa, mbele kwa mbele, kilio na mayowe vikatamalaki nchi yote, mamilioni ya watu wakaingia barabarani hadi mapolisi yakatuchoka, yakawa hayana hamu na sisi tena, Moi akakubali yaishe turekebishe nchi.

Huwa najihisi shujaa maana nilihusika na ninalo kovu mdomoni lililotokana na jeraha la kipindi hicho. Nakumbuka ilikua kama haulow damu au kuathirika kwa mabomu ya machozi ulikua unajiona wa hovyoo, kila mmoja alikua anatafuta apigwe na polisi ilmradi ajihisi amehusika kwenye kuikomboa nchi.
 
Nani kakwambia Watanzania tunateseka
 
Kwani sheria zenu zinaruhusu mtu kuingia kenya bila vigezo[emoji23][emoji23][emoji23].

Na mnatakiwa kufanya nini endapo mamlaka zenu zitashika mtu sampuli hiyo?

Lema hajajitanabaisha kama ni mkimbizi wa machafuko?mhanga wa vurugu za uchaguzi, au mhanga wa haki za binaadam.Na serikali yenu itakuwa dhaifu sana ikikubali mtego dhaifu kama huo.
 
kwani sheria zenu zinaruhusu mtu kuingia kenya bila vigezo[emoji23][emoji23][emoji23].

na mnatakiwa kufanya nini endapo mamlaka zenu zitashika mtu sampuli hiyo???

lema hajajitanabaisha kama ni mkimbizi wa machafuko?mhanga wa vurugu za uchaguzi,au mhanga wa haki za binaadam.na serikali yenu itakuwa dhaifu sana ikikubali mtego dhaifu kama huo.
Baada ya ile movie ya maandamano kushindikana sasa hivi wameambiana waaanzishe movie nyingine ya kukimbilia nchi zingine kwa kigezo eti wanatishiwa,

Yaani ili mradi tu watafute huruma za wananchi.
 
Back
Top Bottom