Kenya yasitisha vibali kwa madaktari wageni wenye vigezo sawa na wazawa

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Serikali ya Kenya kupitia Wizara ya Afya imetangaza kusitisha utoaji wa vibali vya kazi kwa madaktari wa kigeni wenye vigezo sawa na madaktari wazawa ikisema vibali vitatolewa tu kwa madaktari bingwa wa kigeni wenye ujuzi maalum usiopatikana nchini humo ambapo hatua hiyo imelenga kulinda ajira za Wataalamu wa afya wa ndani ya Nchi.

Uamuzi huo umeibua upinzani, ambapo Chama cha Madaktari kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kimewasilisha kesi mahakamani kikipinga hatua hiyo, kikidai kuwa inakiuka misingi ya ajira na uhuru wa kufanya kazi ndani ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Vilevile hatua ya Kenya imezua mjadala mpana kikanda kuhusu utandawazi wa ajira ndani ya EAC huku baadhi wakiona ni hatua halali ya kulinda maslahi ya Wazawa na wengine wakionya kuwa inaweza kuhatarisha mshikamano na ushirikiano wa kikanda katika sekta ya afya.

Kwa mujibu wa Itifaki ya Soko la Pamoja ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC Common Market Protocol), nchi wanachama zilikubaliana kuruhusu uhuru wa watu kusafiri, kuishi na kufanya kazi ndani ya ukanda huo, ikiwemo haki ya wataalamu kutoa huduma zao katika nchi nyingine wanachama.

Hata hivyo, itifaki hiyo pia inazitambua mamlaka za kila nchi kuweka masharti ya kitaifa yanayohusu ajira, leseni za kitaaluma na ulinzi wa maslahi ya umma, hususan katika sekta nyeti kama afya.

Je, uamuzi huu unaweza kuhatarisha utangamano wa jumuiya ya Afrika mashariki ama ni hatua stahiki ya kulinda ajira za wazawa?
 
Attachments

Serikali ya Kenya kupitia Wizara ya Afya imetangaza kusitisha utoaji wa vibali vya kazi kwa madaktari wa kigeni wenye vigezo sawa na madaktari wazawa ikisema vibali vitatolewa tu kwa madaktari bingwa wa kigeni wenye ujuzi maalum usiopatikana nchini humo ambapo hatua hiyo imelenga kulinda ajira za Wataalamu wa afya wa ndani ya Nchi.

Uamuzi huo umeibua upinzani, ambapo Chama cha Madaktari kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kimewasilisha kesi mahakamani kikipinga hatua hiyo, kikidai kuwa inakiuka misingi ya ajira na uhuru wa kufanya kazi ndani ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Vilevile hatua ya Kenya imezua mjadala mpana kikanda kuhusu utandawazi wa ajira ndani ya EAC huku baadhi wakiona ni hatua halali ya kulinda maslahi ya Wazawa na wengine wakionya kuwa inaweza kuhatarisha mshikamano na ushirikiano wa kikanda katika sekta ya afya.

Je, uamuzi huu unaweza kuhatarisha utangamano wa jumuiya ya Afrika mashariki ama ni hatua stahiki ya kulinda ajira za wazawa?
Hii nzuri
 
Back
Top Bottom