Kenya yathibitisha kisa cha pili cha Ebola, mgonjwa wa miaka 39 agundulika akiwa Karantini

Kenya yathibitisha kisa cha pili cha Ebola, mgonjwa wa miaka 39 agundulika akiwa Karantini

Wakaguongo

Member
Joined
Sep 23, 2026
Posts
95
Reaction score
38
1535.jpg

​
Kenya imethibitisha kisa cha pili cha Ebola, baada ya mgonjwa mwenye umri wa miaka 39, ambaye ni ndugu wa karibu wa mgonjwa wa kwanza, kupatikana na virusi hivyo akiwa karantini. Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Patrick Amoth, amethibitisha.

Kisa hiki kipya kinaonyesha umuhimu wa ufuatiliaji wa watu waliokuwa karibu na mgonjwa wa kwanza. Kwa kuwa mtu huyo alikuwa tayari karantini, kugunduliwa kwake kunaonyesha jinsi ufuatiliaji na upimaji wa watu walio katika hatari unavyoweza kusaidia kutambua maambukizi mapema.

Kisa cha kwanza kilihusu Mkenya aliyekuwa akiishi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ambaye alisafiri kupitia Uganda na kuwasili Nairobi Oktoba 3. Alithibitishwa kuwa na virusi vya Ebola na baadaye akafariki Oktoba 5.

Kwa sasa, umakini mkubwa unaelekezwa katika ufuatiliaji wa watu waliokutana na wagonjwa, kutambua maambukizi mapema na kuzuia kuenea zaidi kwa virusi hivyo.

Je, Kenya iko tayari kudhibiti hali hii, na ni taarifa gani wananchi wanapaswa kupewa ili wawe makini bila kuingiwa na hofu?
 
Kutakuwa na visa vingine ukichukulia patient zero alitumia vyombo vya umma katika kusafiri kwake...
 
ila kuna watu wa ajabu, huyo mkenya patient Zero kakaa huko Congo kwenye Ebola baada ya kujisikia hovyo badala abaki huko huko eti linarudi nyumbani kutibiwa, why tena limekatiza nchi ya watu Uganda. ona sasa mabalaa anayosababishia ndugu zake.
 
Serikali ya ruto ilikubali mpango wa Marekani kujenga kituo cha ebola ilihali Kenya haikuwa na huo ugonjwa.Serikali ilishupaza shingo licha ya wananchi kukataa uamuzi huo.Hayo ndio ndio madhara ya kutokusikiliza wananchi malipo yake ndio kama hayo
 
ila kuna watu wa ajabu, huyo mkenya patient Zero kakaa huko Congo kwenye Ebola baada ya kujisikia hovyo badala abaki huko huko eti linarudi nyumbani kutibiwa, why tena limekatiza nchi ya watu Uganda. ona sasa mabalaa anayosababishia ndugu zake.
Ilitakiwa utaratibu wa quarantine uanze mara tu kisa cha kwanza kilipogundulika Congo badala yake wanasubiri usambae ndio wakurupuke kuchukua hatua
 
Ilitakiwa utaratibu wa quarantine uanze mara tu kisa cha kwanza kilipogundulika Congo badala yake wanasubiri usambae ndio wakurupuke kuchukua hatua
How? Karantini inaanzaje? Kama hujagunduà mgonjwa unafanyaje karantini Tanzania. Tuelimishe.
 
Back
Top Bottom