Kenya yathibitisha mgonjwa wa tatu wa Ebola aina ya Bundibugyo

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Kenya imethibitisha mgonjwa wa tatu wa Ebola aina ya Bundibugyo.
-
Mgonjwa ni mwanamke mwenye umri wa miaka 65, ambaye ni ndugu wa karibu wa wagonjwa wawili wa kwanza.

Alikuwa amewekwa karantini baada ya kugunduliwa kuwa miongoni mwa watu walikutana moja kwa moja na wagonjwa wawili wa awali

Soma Pia: Kenya yathibitisha kisa cha kwanza cha Mgonjwa wa Ebola – Mgonjwa Mkenya amefariki

Virusi vya Ebola kwa kawaida huambukiza wanyama, hasa popo wa matunda, lakini milipuko kwa binadamu wakati mwingine huanza pale watu wanapokula au kushika wanyama walioambukizwa.

Chanzo: BBC Swahili
 
3 Kiserikari kiraia ni 30. Walipokea dollar za Marekani ili wajenge wodi za wagonjwa wa Ebola sasa kimewalamba. Ni ngumu mno kupambana na Ebola, Tanzania ifunge mipaka yote na Kenya kwa muda hadi pawe shwari.
 
Wakenya wanajitengenezea mazingira ya kutoruhusiwa kuingia baadhi ya Nchi nilikua na mpango wa kwenda Nairobi ila naona wataharibu safari zingine wataanza kuuliza kama umeenda Kenya au DRC hivi karibuni ukijibu ndio na wakiona mkwaju unawekwa karantini yao mpaka wakupime kutoka sio leo.
 
Kaa utulie tu boss wangu.
Hivi ni viashiria ambavyo vimeanza sahizi kila mipaka itaanza kuchukua tahadhari
 
Aiseeee Mungu tuokoe ,hatari sana!
 
Usiende, jana niliishia mpakani kuna heka heka si ndogo nikageuza, kuna kamchezo kanataka kufanyika, wabongo tuwe makini
 
Usiende, jana niliishia mpakani kuna heka heka si ndogo nikageuza, kuna kamchezo kanataka kufanyika, wabongo tuwe makini
Ok ikishakua hivyo siendi maana nilitaka kwenda Nairobi harafu niende SA kupitia huko pia nikaja kugundua kuwa ntasumbuliwa Oliver Tambo nasikilizia wiki ijayo ntatoka kupitia daslm maana sisi kutangaza hizi mambo sio leo..
 
So mr kasongo ame aim zaidi kwenye misaada

Vilevile kulinda watu wake...

Tulifichaga Covid hapo kwetu, uliona msala iliyouleta hadi kwa namba 1 😃
 
Hii itakua mbaya sana, Nasubiri visa nieleke Japan na Nina mpango wa kupitia Nairobi cause price ni cheap kuliko kutokea Dar.
Sasa kwa Hali hii inaweza vuruga kila kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…