Kenya yathibitisha mgonjwa wa tatu wa Ebola aina ya Bundibugyo

Kenya yathibitisha mgonjwa wa tatu wa Ebola aina ya Bundibugyo

Yes, Ila China Southern via Guangzhou ilikua poa sana ticket in 2.5M go and return.
Na ukizingatia hapa mpaka Nairobi sio mbali na ndege ni cheap.
Cathy pacific ticket ni 2.8M ila kutoka Dar To JNB Kuna umbali kidogo.
Ila kwa Hali ilivyo Kenya Sina budi.
Ukikata mapema zaidi utapata nafuu ya hapo kwa hiyo Cathy unachofanya unakata ticket ya mapema zaidi Malawi au Rwanda wapo cheap unaenda kufanya transit Oliver Tambo au ukiamua unakata siku moja kabla siku inayofata unaanza safari hapo Oliver Tambo..
 
Kenya imethibitisha mgonjwa wa tatu wa Ebola aina ya Bundibugyo.
-
Mgonjwa ni mwanamke mwenye umri wa miaka 65, ambaye ni ndugu wa karibu wa wagonjwa wawili wa kwanza.

Alikuwa amewekwa karantini baada ya kugunduliwa kuwa miongoni mwa watu walikutana moja kwa moja na wagonjwa wawili wa awali

Soma Pia: Kenya yathibitisha kisa cha kwanza cha Mgonjwa wa Ebola – Mgonjwa Mkenya amefariki

Virusi vya Ebola kwa kawaida huambukiza wanyama, hasa popo wa matunda, lakini milipuko kwa binadamu wakati mwingine huanza pale watu wanapokula au kushika wanyama walioambukizwa.

Chanzo: BBC Swahili
Naomba EBORA IFIKE ZANZIBAR
 
3 Kiserikari kiraia ni 30. Walipokea dollar za Marekani ili wajenge wodi za wagonjwa wa Ebola sasa kimewalamba. Ni ngumu mno kupambana na Ebola, Tanzania ifunge mipaka yote na Kenya kwa muda hadi pawe shwari.
Nakazia hili ila utakuta nchi ipo bize kupambana na upinzani, Ebola ni hatari.
 
AFCON 2027,tutabaki vya viwanja na nyumba za hotel na Kulala
Inasikitish sana na hizo dalili ni kama hilo jambo litaenda kutokea, Tz ipo bize kupambana na upinzani.

Ebora ikiingia hapa Tz na kwa maisha yetu yalivyo hasa Dar es Salaam, mbona watu tutapukutika sana.
 
Ruto mhuni sana anataka kuuchezea uchaguzi mwakani taratibu anaanza kudondosha meza
 
Nina kila kitu kwa ajili ya safari ya Nairobi kwenda Standard Chartered Nairobi Marathon 2026 na safari ni tarehe 23, lkn naona ishakuwa noma!!!
 
3 Kiserikari kiraia ni 30. Walipokea dollar za Marekani ili wajenge wodi za wagonjwa wa Ebola sasa kimewalamba. Ni ngumu mno kupambana na Ebola, Tanzania ifunge mipaka yote na Kenya kwa muda hadi pawe shwari.
Ni hatari kwa kweli. Bahati mbaya sijui kama kuna maandalizi ya kutosha kukabiliana na hilo tatizo.
 
Back
Top Bottom