Kenya yaweza fikisha 10% kwa ukuaji wa GDP 2022

Kenya yaweza fikisha 10% kwa ukuaji wa GDP 2022

Nairoberry

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2012
Posts
932
Reaction score
525
Hivi sasa manake upinzani umetulia na wanafanya kazi kwa kushirikiana na serikali, Kenya iko mbele, Rais Uhuru amechukua hii nafasi kutia bidii sana kukuza uchumi wa nchi, mwaka ujao ukuaji wa uchumi utafika 6% kulingana na mashirika mbali mbali. Uhuru amealikwa Canada kwa mkutano wa G7 na atatumia iyo nafasi kuiuza Kenya kabisa katika uwekezaji zaidi. Hali hii ya utulivu Kenya ni mwafaka sana kwa kufanya biashara na kuiendelesha nchi sana, kipindi kijacho cha miaka minne kabla uchaguzi tuna nafasi nzuri kwa mara ya kwanza kufikisha asilimia 10 kwa ukuaji wa uchumi. kipindi cha mwaka wa 2007 kabla ya uchaguzi Kenya ilifikisha asilimia 7% na kusambaratika baada ya machafuko yaliyotokea na uchaguzi kufika tu 1%, kama ilo halingalitokea Kenya sasa ingalikuwa na 18% kwenda juu ya ukuaji wa uchumi.
Wakenya tumekuwa kila uchao tukijilinganisha na nchi kama Singapore,Korea Kusini na Malaysia, sioni mbona sasa hatuwezi piga hatua nzito mpaka angalau kufikisha GDP yetu $ Billioni 150 mwaka wa 2022. hichi kipindi kuanzia sasa Uhuru anapaswa kuhakikisa ni maendeleo tupu hamna kizingiti ata kidogo.
Ebu Mungu tusaidie, kwa sababu wewe unasaidia wale wanajisaidia.
 
Nawaza kwa sauti izo wish ziwafikie na wale juakali sio wachache tu waneemeke na huo mkate..All the best
 
Back
Top Bottom