Kenyaforum: Who is your best conversationalist?.

Aisee bro Kimweri yupo wapi?
 
Kuna Xplorer pia alikuwa analeta michango katika pipeline saga leo kesho unaona alichozungumza kimekuwa kweli mpaka at times the East African walikuwa wana-source details toka kwake indirect lazma yupo sehemu nyeti alichokuwa anazungumza kilikuwa kinakuwa kweli.
 
MK254 unamkumbuka Dr. Job?
huyu ni mmoja ya wakenya wale ma-great thinker waliotamba sana hapa jf.

siku hizi simuoni,naweza sema alikuwa na u-genius fulani katika mada zake japo nyingi zilikuwa hazimuingi mkono uhuru kenyatta.

kuanzia kingereza chake mpaka point zake,jamaa alikuwa anaonyesha sio mtu wa kawaida katika kufanya naye mjadala.Mimi nilikuwa naishia tu kusoma comment zake na kuhepa kimya kimya.[emoji23] [emoji23]

kuna kipindi niliona ulikuwa unajaribu kupangua hoja zake.[emoji23]

moja ya kazi yake ni hii hapa.
 
kiboko yake na NairobiWalker[emoji23] [emoji23] (utani kidogo).....dr.kimweri nahisi kapewa idara nyeti huko serikalini.maana yupo kimya sana siku hizi.
Hamna topic niliyopenda kuchangia kama Uganda's pipeline maana majadiliano yalianza toka JK era mpaka JPM anakamilisha deal. Ningependa kama Uongozi wa JF wangerudisha yale majadiliano maana yalikuwa mazito nina uhakika kama watu tungekuwa tunaonana uso kwa uso, tungeshikana mashati..
 
baraza la kiswahili tanzania (bakita) juzi kati waliibuka na kudai kuwa mchanga wenye madini hauitwi "makinikia" bali huitwa "MASHOBO".[emoji23] [emoji23]
Wako sahihi, maana MASHOBO ni mabaki ya kitu fulani. Na ule mchanga ni mabaki baada ya uchambuzi wa kwanza.
 
[emoji23] na kweli, mashati yange shikwa. Shikamoo mtandao.
 
Nilishaliona hilo siku nyingii..jamaa ni nationalists waliopitiliza..
 
bora tubaki hivi hivi hatufahamiani kwa sura maana wengine huwa tunatembelea sana huko kenya kwenye shughuli zetu mbalimbali.

watu wanaweza wakakutegeshea vitu vyenye ncha kali pale boda ya namanga[emoji23] [emoji23]
Kweli kabisa, wengine tunatia mguu Kenya kama nyumbani kwetu, wakitujuwa utarudi bila meno [emoji16] [emoji16]
 
Nilishaliona hilo siku nyingii maana jamaa ni nationalists waliopitiliza...
 


Hehehe!! Kaka tatizo ulikua husomi mada kikamilifu na kutofautisha wakati mtu amecopy paste taarifa kutoka kwengine au kaandika mwenyewe neno kwa neno. Huyo Dr Job sijaona sehemu ameweka bango lake mwenyewe zaidi ya sentensi tatu. Kuna watu huwa ni mamluki wa kuokoteza taarifa na kuzipaste kwenye mitandao ya kijamii halafu hawarudi tena kutetea hoja yenyewe watu wakianza kujibu, maana yupo kikazi hivyo lazima afikie tovuti kama hamsini kwa siku.
Hiyo hapo aliyoweka Dr Job alinyofoa kutoka kwa nakala ya Onyango Oloo na kuiweka humu bila kuweka na chanzo pia, akaishia kuwafanya mkadata, hebu ifuate huku http://allafrica.com/stories/201110281060.html

Humu kuna watu wasioendana na Uhuru kenyatta, ambao hawatampa kura na ni mashabiki na wafuasi wa Raila, lakini wakiandika makala unaona wamedhihirisha uelewa wa ndani na wanatetea hoja zao ipasavyo. Kwa mfano Sammuel999 akianza kukosoa serikali ya Jubilee huwa naishia kumkubalia kwenye kila neno maana hata kama yeye shabiki wa Raila, lakini ana mantiki kweli kweli.

Lakini watu wa ku-copy paste makala bila kuweka chanzo halafu wanatoweka hawatulii kutetea pale wadau wakianza kujibu, kisha watarudi baada ya miezi kadhaa na bandiko lingine huwa siwafagilii. JF kuna wakati ilikua inanoga, nilikua napenda sana kwenda kwenye mada za kimataifa, Great Thinkers, Jamii Intelligence, Jukwaa la Siasa n.k. Maana kule ndio nilikumbana na Watanzania wanaojadili hoja hadi zinatulia, lakini siku hizi wengi wametoweka.

Halafu kuna wadau kadhaa hata huku kwa Kenyan forums ambao walitoweka, tulikua tunapelekana hadi kinaeleweka. Siku hizi ni vigumu kumkuta mtu ambaye ninaweza kujadili naye hadi kuchochea mawazo yangu.
 
what if the guy who calls himself dr job in jf is onyango Oloo?.

kaka jf ni kama kichaka kizito.mda mwingine ili kugundua huyu ni nani inabidi tu ujiongeze wewe mwenyewe au uunganishe dot.[emoji23]
 
Kafrican,

Nivlark,

Sammuel999 and his younger, less sentimental brother, sam999 (dont kill me Sam, I didnt say u are sentimental),

MK254, the arch- debator on the Jf Kenya, his brilliant command of both languages and profound grasp of a wide array of issues has made him quite a legend here,

Mwanzi1,

Geza Ulole, Kenyans may not like him but c'mon, he' s good,

Kimweri- I dont know when he will finish his jail term, but he's also frighteningly good,

Econometrician,

EngineerLMG,

Edward Wanjala

kui,

I dont know if Jack Daniel's is still alive. Bad quidnunc!

Tobaa,

Mwanzi1,

JokaKuu

and not forgetting NairobiWalker, who is currently in Nigeria, battling them on on their own forum.
 
Annael na lusematic nafurahi sana kuwaona huku
 
binafsi Mimi huwatambua sana geza ulole na mk254 not forgetting samy999 fighting spirit of you guys is on another level.. can't mind to throw one two to you guys.keep it up guys
 
Shukrani Iconoclastes Geza hoja zake huwa nzuri kuna wakati anajibu mpaka mwenyewe unaona point.
MK254
Iconoclastes
Livale
Edward Wanjala
1africa
Kafrican
Samuel999
Tuusan
sijui mbona mnasahau Dhuks
Nairobiwalker kuna mcoast fulani sijui ni saadik nimesahau jina.
Waliofanya niingie JF ni Geza,Dhuks NairobiWalker na Kafrican
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…