Kenyan media houses against Tanzania

Dah! Kingereza cha Wabongo...hehehe haya bana.

Anyway sio Kenya tu, mnasemwa kote hadi na WHO, mbinu zenu ni kinyume na mataifa yote ya dunia, mnasuasua kutoa data na kuwapa watu wenu matumaini hewa, kisha mnashtukiza na namba za kiajabu na kuwaacha hoi.

Wenyewe mnapima watu wachache kwa siku lakini tayari mumeongoza EAC kwa idadi ya maambukizi, hiyo tayari inaonyesha jinsi gani mnacheza mchezo hatari.

WHO yailaumu Tanzania kutokutoa ushiriano mzuri takwimu za COVID19 - JamiiForums
 
Umesema ukweli mtupu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora wakenya mtusaidie maana media za huku zimewekwa mfukoni
 
Hivi WHO imesema kwamba lazima kila nchi itoe data kwa kila Siku au kila nchi inajipangia utaratibu wake?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi WHO imesema kwamba lazima kila nchi itoe data kwa kila Siku au kila nchi inajipangia utaratibu wake?

Sent using Jamii Forums mobile app

Hili ni janga la dunia, lazima tufuate template inayoeleweka, nyie wenyewe hapo bila aibu mnaomba misaada mabeberu ilhali bado mnataka mfanye mambo yenu yasiyoendana na mantiki yoyote, data za nini unakaa ndani nazo, hii hata mabingwa wa kuficha data akina China na Urusi wote wanataarifu hali yao, nyie na umaskini wenu wa Kiafrika mnasuasua ya nini halafu mnakuja kushtukiza na kupita majirani zenu wote kwa idadi ya maambukizi.

Halafu nyie ndio nchi ambayo mpaka leo mnakusanyika kwenye vilabu vya pombe, majirani zenu wamewafungia mipaka maana nyie ni wakaidi na wabishi kuliko maelezo, mnapukutika hadi wabunge na bado mnaendelea kukaidi, namba za waathirka wenu zinapandisha kwa kishindo ilhali mnapima watu wachache sana na bado hamuoni kama issue.
Mngekua mnapima kwa kasi kama majirani zenu yaani ndio mngeelewa nini kinaendelea duniani.
 
Tatizo ninaloliona kwa wakenya ni kutaka kuifanya Kenya ndio iwe ni "Benchmark" katika kila jambo.

Mwanzoni wakati idadi ya wagonjwa Tanzania in ndogo kuliko Kenya, mlisema sababu kubwa ni kwamba Tanzania haipimi wagonjwa wengi. Sasa hivi idadi ya wagonjwa Tanzania ni kubwa kuliko Kenya, bado mnakuja na sababu zingine ili kutaka kuthibitisha kwamba Kenya siku zote ndio ipo sahihi katika kila kitu.

Mimi ninashauri kwamba kila nchi ifanye inavyodhani inafaa kwa watu wake, ilimradi isitoke nje ya maelekezo ya WHO. Kama una ushahidi wa Tanzania kutofuata ushauri wa WHO tafadhali tuambie ili tujifunze.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Wala sio Kenya ndio benchmark, kirusi hakijaanzia Kenya, kimetukuta sote na tunafuata benchmark zilizopo duniani, pili bado namba zenu mnapima wachache kuliko majirani zenu wote, hata Rwanda kataifa kadogo kanawazidi kwa idadi ya vipimo kwa siku, niliona eti juzi ndio mnasema mumefikia uwezo wa kupima 500 kwa siku, na ikumbukwe sio kwamba ndio mnapima hao, la ila ndio mumefikia huo uwezo, wakati sisi wengine tunachezea kwenye kupima maelfu.

Sasa ukizingatia mnapima wachache na bado mnaongoza ukanda wote huu kwa idadi ya maambukizi, je siku mkipata uwezo wa kupima kama sisi si ndio mtashangaza hadi dunia.

Acheni ukaidi na ubishi usio na tija, zingatieni ushari na maelekezo ya kisayansi, pima pima pima, chukua tahadhari, fungeni maeneo ya kijamii yasiyo ya lazima, vilabu vya pombe havina umuhimu wowote zaidi ya watu kupumuliana virusi, kwanza mlevi akishalewa anatupa barakoa kule na kuanzia hapo hajali chochote.

Mombasa yetu naona namba zinapandisha sana, nashuku ni huo ujirani na undugu wao na Tanzania unaweza kuwa unawaponza, maana hata ukifunga mipaka haimaanishi ndio umeweka ukuta baina ya Wadigo na makabila yote tunayochangia kwenye mipaka. Bado watahusiana kila siku tena kwa maelfu....full nyomi
Hivyo hatuna jinsi ila kuwasema pale mnazingua na kutoonekana kujali na kuponza kanda zote za EAC na SADC.
 
Vipi kuhusu Uganda ambao wamepima watu wengi zaidi ya Kenya na bado maambukizi ni machache sana?, nani anayesema ukipima watu wengi lazima upate maambukizi mengi?, Uganda wastani kwa siku wanapima watu 1500 na hawapati hata muathirika mmoja.

Tatizo bado wakenya mnadhani kila mnalifanya ni sahihi na wengine hawako sahihi. Tanzania wanafanya " strategic testing" ndio sababu wanauwezo wa kugundua wagonjwa wengi kwa vipimo vichache, wakati Kenya mnajipimia kiholela bila kutumia akili, vipimo vingi vinatumika kwa watu ambao sio lazima kupimwa.

Kenya mnapaswa kufanya vile muonavyo ni sawa kwa nchi yenu, na muache Tanzania ifanye vile inavyoona ni sawa kwa upande wake, ili muradi haitoki nje ya maelekezo ya WHO.

Kuhusu mikusanyiko, hivi Kenya hakuna kwenda Sokoni, hamuingii katika vyombo vya usafiri?, Likoni ferry haifanyi kazi?, au katika nyumba za ibada ndio sehemu pekee watu wanakusanyika lakini sio Sokoni, katika public transportation, Supermarkets, offisini, Ferry na hata mijini ambako kote kunaruhusiwa huko Kenya?. Acheni tabia ya kujifanya ninyi ndio mko sawa kwa kila Jambo.

Kama kuna nchi za kujifunza, ni Kenya na Tanzania kujifunza kwa Uganda na Rwanda, ndio sababu hata idadi ya watu wagonjwa na vifo inaonyesha hivyo, Kenya na Tanzania hakuna anayefanya vizuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Uganda pamoja na kupima wameongeza hatua moja zaidi yetu, wamepiga kitu kinaitwa "full lockdown", Museveni na Kagame wametokea jeshini, hawana hulka ya kucheka na kima, wakitoa amri sharti zifuatwe, kwao huko kila mtu ndani, hivyo maambukizi yao bado yapo chini.

Nyie hapo mumechanganykiwa, kila mtu na lake, mara RC wa Dar aseme mchape kazi haogopi corona, mara aambie watu wa mikoani wasije Dar maana watu wanapukutika, mara anunyize dawa, mara asemwe na rais kwa hilo la dawa na kusemwa kwamba ndio linasambaza corona, mara rais aseme corona haingii kanisani itaungua, mara rais aseme barakoa ndio zinakuja na corona, mara aseme waliopona ni zaidi ya mia huku waziri mkuu akisema waliopona ni 11...yaani nikiandika mnavyojikanganya nitapoteza muda sana hapa.

Mnapaswa kujifunza jinsi ya kupambana na janga na kuacha ukaidi, kwanza na muhimu kabisa ni kuwaskliza wataalam wa kisayansi maana janga lenyewe ni la kisayansi sio kufuata hisia na mihemko.
 
Mbona nime kusahihisha mara kadhaa humu! Hii sio lugha yako, waache wajifunze.

Huna jeuri ya kunirekeisha maana wewe kwanza sijawahi kuona umeandika chochote cha maana zaidi ya matusi, ukishajifunza tusi la kingereza lazima uje kasi kulitupia humu.

Mimi binafsi huku JF huwa nachangia kwa Kiswahili maana walengwa wameaminishwa kwamba kuongea au kuandika kwa kingereza ni utumwa, hivyo huwa kinawapa changamoto sana. Lakini nikiwa kwenye forums za Wakenya au kule Quora, huko huwa nachangia kwa Kingereza.
 
Mie ni mtanzania ila we are absolutely wrong in the manner we are handling the Covid-19 pandemic.

Katika kila sekta huwa kunakuwa na models za jinsi ya kudeal na challenging issues. Uchumi, afya, ulinzi vyote hivyo vina operating models ambazo ni internationally and professionally accepted.

Kwenye issue ya pandemic suala la kutoa data sahihi na kwa muda mfupi iwezekanavyo ni moja ya models zinazotakiwa kufuatwa.

Unfortunately, hali tukijua umuhimu wa hizo models hatuzifuati, sio kwa matakwa ya wataalam wetu bali ya wanasiasa.

Ndio maana nawaunga mkono wakenya wanapotuona we are so primitive japo sio wote, some of us we are in our perfect state of mind.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eti "strategic testing", ndio nini hiyo, acha kushabikia ujinga.

Yaani mpaka mtu augue ndio umpime, hapo atakuwa kaambukiza watu wangapi. Usitufanye watanzania wote wajinga kwa uzembe wa wanasiasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Trust me we know so many of you that are sober minded, i have friends till todate they have been in quarantine and are taking this this illness very serious, the problem comes in that majority of your country people are blinded by Ujamaa and are unable to question your government, whatever the government says they dont mind even if people are falling in the streets

Sent using Jamii Forums mobile app
 
First, as a Kenyan i look down upon Tanzania to orient myself on how not to do things. Second, Sawahili has got nothing to do with Tanzania if you are a student of history
 
Kenya na Tanzania wote hakuna anayefanya vizuri, huko kwenu POLISI wanauwa wakenya kuliko Corona, Mara watu wanakanyagana kwa kugombea chakula cha msaada, Mara waliopo Karantini wanajiua, Mara wanaruka ukuta na kukimbia, Mara pesa ya kupambana na Covid waziri na watendaji wake wanazitumia kwa kununua vocha za simu, Mara wanazinywa chai, Mara hivi, hamuishiwi vituko.

Njia pekee inayoonyesha kufanya Nazi katika kudhibiti maambukizi ni " total lockdown " huko kupima watu wengi hakusaidii chochote, USA wanakaribia kupima watu milioni 6, lakini maambukizi na vifo ndio vinaongezeka.

Tokeni vichakani na mkubali kwamba Kenya haifanyi vizuri kama ilivyo Tanzania, hizi nchi zinafaa kuiga Uganda na Rwanda, hiyo habari ya kwamba " total lockdown " huwekwa na vipngozi wanajeshi pekee ni sehemu ya kutafuta sababu ya kushindwa, South Africa,, Botswana na nchi zingine nyingi zilizo chini ya " lockdown " nao viongozi wao ni wanajeshi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Nimeona kuna Watanzania humu wamekujibu vizuri tu, sina haja ya kuhangaika na wewe zaidi maana ni dhahiri kuna Watanzania wanaotumia akili, hivyo kwa mimi kuendelea kuwajumuisha wote kwa akili za mtu mmoja nitakua nawakosea heshima hao, wacha niwaachie uwanja waendelee kukupa darasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…