Tume iliyoundwa kuchunguza ajali ya helikopta iliyosababisha kifo cha aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani wa Kenya Profesa George Saitoti na watu wengine watano, imesema kuna uwezekano mkubwa kuwa ajali hiyo ilisababishwa na makosa ya rubani.Hakuna mtu aliyenusurika ajali hiyo iliyotokea katika mji wa Ngong nje kidogo ya jiji la Nairobi.
Kiongozi wa tume hiyo Kalpana Rawal amesema kuwa huenda helikopta hiyo ilianguka baada ya rubani kushindwa kuidhibiti kutokana na ukosefu wa mwanga wa kutosha.Mjumbe mwingine wa tume hiyo Peter Maranga amesema inawezekana marubani wawili wa helikopta hiyo hawakuwa na uzoefu wa kutosha kuendesha ndege katika hali mbaya ya hewa.
Aidha tume hiyo imesema imegundua hitilafu katika sekta ya mafunzo na ubora wa kiufundi katika ndege.Hali kadhalika tume hiyo imeilaumu kampuni ya Eurocopter iliyoiunda helikopta hiyo, kwa vipuri ilivyowekewa ndege hiyo siku chache kabla ya kuuzwa kwa polisi nchini Kenya.
maelezo yako ayaendan na mtangazaji wa eatv ambaye amesema ajali ilitengenezwa na watu wazito toka serikalini na baada ya ile ndege kuanguka na watu kupoteza maisha mmoja wa watu waliofika kwenye tukio walichukua simu ya prof saitoti na kuanza kuitumia kwa kuwasiliana na mkubwa mmoja serikalini na inavyo semekana uwenda wale marubani walipoteza maisha kabla ya ndege kuanguka
Kwa sababu hizo wanasema uwenda watakuwa waliwekewa gas ya kuua na ndipo walipoivuta wakapoteza maisha na ndege kupoteza muelekeo na kuanguka
Kama unangoja utajiwe kwamba huyu ndie muhusika mkuu,basi ngoja sana mana hutaelewa kitu,lakini wabunge wameona,na utaona vile bunge litawaka moto ju ya swala hili,ile gharama imetumika kwa ajili ya uchunguzi huu,alafu wewe unaubeza!!!,.
Its now very obvious that Saitoti was murdered by the closest confidants to the current President...'the Butcher of Naivasha'...the man is coming into office with his hands dripping of both old blood (post '07 PEV) and new blood (this Saitoti debacle.)...Who is going to save Kenyans from this ogre!