Ninasoma hili jibu lako, nimerudia mara nyingi lakini sijakuelewa kabisa, sijui unataka kuzungumza nini hapa. Bajeti ya taifa inaonyesha projection ya matumizi, kwamba mwaka huu Kenya inategemea kutumia pesa nyingi kuliko Nigeria, sasa mfano wako wa mapato ya vyumba unakujaje hapa?
Nyinyi mnaishangaa Nigeria kupanga kutumia pesa kidogo kuliko Kenya, kwamba Kenya yenye uchumi mdogo imepanga kutumia pesa nyingi kuliko Nigeria yenye uchumi mkubwa, tena pesa nyingi zinatumika kulipia mishahara sio miradi ya maendeleo, tena Kenya hiyohiyo inayopanga kutumia pesa nyingi kwa kulipia mishahara deni lake ni 54%, wakati Nigeria yenye uchumi mkubwa na deni la 18%, Bado inajitahidi kubana matumizi kwa kupanga bajeti ndogo zaidi, pamoja na kwamba inawafanyakazi wengi zaidi ya mara nne ya idadi ya wafanyakazi wa Kenya wanaolipwa mishahara. There must be something wrong in Kenya, very difficult to understand this scenario