Unajua hapo ndo tunatakiwa kubadilika. Kama mtu anamawaa kwanza tuakikishe tunasafisha bala letu then ndo tuanze kulalamika ...kwa kweli Afrika tumezalisha madikteta wengi sana. Kuna mmoja yeye nahisi ni wa Kwanza kwa unyama huyu si mwingine bali rais wa Equatorial Guinea. Jamaa anagereza [kabla ya hapo alikuwa mkuu wa gereza hili kabla ya kumpindua mjomba wake 1979] linatwa 'Black Beach' Ukiingia humo ni balaa! Nchi yake ina watu laki sita na ni ya tatu kwa kuzalisha mafuta kusini mwa jangwa la sahara lakini ni masikini wa kutupwa na huyu dikteta ni tajiri wa kutupwa