Haki hutafutwa Wakenya walipofikia hawakungoja ifike siku wapate katiba mpya viongozi wetu wameshalewa madaraka hawaoni sababu ya wao kutengeneza mianya ya wengine kuitwa ma bwana wakubwa. Hakika wakenya wana stahili pole kwanza kabla ya pongezi. Pole kwa kupoteza mamia ya wakenya baada ya uchaguzi mkuu wa 2007 wa Rais na wabunge ulioleta umwagaji mkubwa wa damu na ndio leo hii umwagaji huo umesababisha Katiba mpya ya kenya.
Swali langu dogo kwa wenye nchi hii waheshimiwa mnataka yaliyotokea Kenya yatokee Tanzania ndio na sisi tupate Katiba mpya? chondechonde wapendwa sisi tuna hamu ya kuishi kama nyie kueni waungwana.
Kwa kumalizia Hongereni Wakenya kwa hatua mliyopiga nyie ni mfano wa kuigwa kwa bara zima la Africa.