Mkuu unafeli!
Labda uniambie idadi kubwa kwenda ivy...Ila eti hata kama ni mmoja kaenda Ivy ndio shule bora?
Nilisoma Ilboru,kuna vitoto hua vinaenda MIT,Harvard,Yale....Ilikua walao kwa mwaka anaenda mmoja,shida ni kua the remaining 99% ni Udsm,sasa kwako hiyo ni shule bora kiivyo?....Na kumbuka hao naturally gifted students hata wangesomea chini ya mti angepata masomo yote A,shida ndio hiyo!
Tusichukulie vitoto vi-genius naturally vimepita shule zetu hizi vikaenda MIT then tuseme hiyo shule ina elimu bora!
Mkuu,
Nilikuwa naongelea idadi kubwa ya wanafunzi kupewa full academic scholarship Ivy League schools.
Pia, kuna quota kwa kila nchi katika shule zao. Hawachukui kila mwombaji hata kama ni top 10 wa darasa lako.
IST kila mwaka, inapeleka sio chini ya wanafunzi 10. Hawa ni full scholarship ambayo ni sawa na $70,000 kwa kila mwanafunzi, kwa mwaka.
Kumbuka kuna raia wa nchi 60 IST. Raia wa nchi zilizoendelea, wao mara nyingi huenda kwao kwanza halafu utamsikia kaenda Wharton kuchukua MBA. Wengine wameridhika na elimu bora za nchi zao.
Watoto wa ubalozi wa nchi masikini wengi pia wanakwenda kusoma Marekani kupitia IST, hata kwa kujilipia.
Pia, sio wote waliosoma wanapewa full scholarship. Shule za Ivy League pia wanaangalia uongozi wako, community service skills na jinsi gani unaandika barua ya maombi na essay yao. Barua ya kuombewa pia inatayarishwa na shule (letter of recommendation) kwa niaba yako. Kama wazazi wana uwezo, unaombwa pia kulipa fee kidogo kuwasaidia wengine.
Katika IB program tunapelekwa kupiga rangi mahospitali kama ocean road, kufagia au kufundisha kiingereza watoto vilema wa shule ya Salvation Army (saba saba). IST pia inaendesha hospitali ya wananchi wenye ukoma. Huwa tunaenda huko kila mwaka kusaidia na kuwaelimisha wanakijiji wa Kindwitwi, kuwa ukoma hauambukizi. Wamewatenga wanakijiji walio na ukoma. Imani za kichawi inasumbua.
Kupata IB diploma, lazima ujitolee masaa 80 kusaidia jamii.
Pia, kusoma ni bidii yako pia. IST inatoa scholarship kwa wanafunzi wa shule za serikali kila mwaka ili wasome IB. Wengi wameweza kupata full au partial scholarship kusoma nje hata kama wamesoma miaka miwili tu IST.