Kwanza ifahamike nchi yetu tunafuata ruwaza 2030 ya taifa, iliandaliwa kitaalam na kizalendo na kila kiongozi ajaye anahitajika kutekeleza shughuli zake kwa kuizingatia hii ruwaza. Hivyo rais Uhuru anachokifanya ni kufuata yaliyo andaliwa awali yake.
Kwa mtazamo wangu binafsi, nimesema binafsi kabla hawajaja wengine kunikomoa...naona tunamhitaji amalize kazi aliyoanzisha, kwa kweli ametuangusha kwenye vita dhidi ya ufisadi, japo pia kama ninavyowafahamu Wakenya, hatupo tayari kwenye hivi vita. hatua zikichukuliwa, viongozi wanakimbilia wafuasi wao na kulilia huko, nawaza hapa leo hii Uhuru akamfuta naibu wake Ruto kwa sababu za ufisadi.