Kenyatta amfokea Rutto hadharani

mwananyaso

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Posts
2,995
Reaction score
3,401
Nairobi, Kenya. Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ameapa kuanza kampeni ya kuzima wanasiasa wa kundi linalo hujumu uongozi wake maarufu kama (Tangatanga).

Rais Kenyatta aliyekuwa akizungumza na waumini wa dhehebu la Akorino katika Uwanja Kasarani Jumapili iliyopita alionekana mwenye hasira na kutumia lugha ya Kikuyu.

Rais Kenyatta alionekana kuwalenga wanasiasa ambao wanamuunga mkono Naibu wa Rais, William Ruto kuwania urais mwaka 2022.

“Leo ninazungumza kwa lugha ya nyumbani, nitaenda katika eneo langu (la Mlima Kenya) kuwaambia watu kile ambacho wanafanya.

“Wanafaa kujua kwamba si wao walionifanya kuwa Rais, bali mimi ndiye niliyewafanya kupata viti. Wakenya ndio walionichagua na nitaendelea kusimama na ukweli hadi nikamilishe kazi mliyonipa.

“Wanafikiri kwamba nikiwa kimya, wamefaulu kuninyamazisha, nimesema kwamba sitaki siasa na hiyo ndiyo maana sijawatimua katika maeneo waendayo,” alisema.

Alisema baadhi ya wanasiasa hasa wa chama cha Jubilee, wamekaidi wito wake wa kutaka wasitishe kampeni za mapema na badala yake watumikie Wakenya.

Kenyatta alisema viongozi hao ‘wakora’ wamekataa kuunga mkono juhudi zake za kutaka kuunganisha nchi kupitia kukutana kwao na Raila Odinga walipopena mikono maarufu (handisheki).
 
Wanasiasa ambao alikuwa anawalenga sio naibu rais William Ruto wala wale ambao wanamuunga mkono. Bali ni wanasiasa kutoka chama chake. Wabunge kutoka maeneo ya Ml. Kenya ambao huwa wanamkashifu wakisema kwamba amewatelekeza.
 
Huyu Kenyatta ni kiongozi mzuri sana, japo nabii hakubaliki kwao ila ukiangalia nyendo zake unaona kuna kitu ndani yake.
Kumbe kufoka kwa kiongozi ni jambo la kawaida, sema tafsiri za watu ndio tatizo
 
Wanasiasa ambao alikuwa anawalenga sio naibu rais William Ruto wala wale ambao wanamuunga mkono. Bali ni wanasiasa kutoka chama chake. Wabunge kutoka maeneo ya Ml. Kenya ambao huwa wanamkashifu wakisema kwamba amewatelekeza.
The Same hapa bongo
 

Bora yeye anaekemea "tangatanga" kuliko wetu anae create tangatanga original na kuwafanya washindwe kufanya hata maamuzi.
 
Huko Kenya wanasema bora ya wakwetu kuliko wakwao, ni mtizamo tu

Sio mtazamo; ila ni reality. Sijaandika nilichoandika kwa kuwa sijui upande huo ukoje (ninafahamu hadi Kibera, Area 3, Buruburu na Baba Dogo). I can guarantee you this fact: Mkenya yeyote anaeitamani Tanzania ni kwa kuwa kuna opportunities za yeye kupata utajiri huku kuliko kwao (na wanamshukuru Magufuli kwa fyongo zake maana zinawarahisisha kupata utajiri) but NEVER kwa kuwa wangetamani watawaliwe na mtu sampuli ya Magufuli.
Of course si kila Mkenya ni smart; they have their own fare share of imbeciles ambao wanaweza kuwa wanatamani ulichokiashiria.
 
Naona unatumia nguvu nyingi kupandisha Chart ya Uhuru na kumbeza Magufuli, anyway ndio akili yako uwezo wake wa kufikiri umefikia hapo ,pia ukitawaliwa na chuki binafsi
 
Unaona unatumia nguvu nyingi kupandisha Chart ya Uhuru na kumbeza Magufuli, anyway ndio akili yako uwezo wake wa kufikiri umefikia hapo ,pia ukitawaliwa na chuki binafsi

Sihitaji kumpandisha chart mtu yeyote. Hivi kuna mtu anaeweza kuipandisha chart Tanzania ikawa juu ya US, au kumpandisha chart Samata akawa zaidi ya Messi? Je, kuna mtu anaweza kuibadilisha Jumatano ikawa Jumapili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…