Kenyatta asita kwenda kikao ICC

Kenyatta asita kwenda kikao ICC

Viol

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
25,420
Reaction score
18,298
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta,amesema kuwa
hawezi kuhudhuria kikao alichoagizwa kuhudhuria
na mahakama ya kimataifa ya ICC mwezi ujao
kutokana na kazi nyingi aliyonayo.
Mahakama hiyo ilimtaka afike mbele yake kujibu
madai kuwa serikali yake imekataa kuwasilisha
shatakabadhi zinazohitajika na mahakama hiyo
katika kesi inayomkabili.
Kenyatta kupitia kwa mawakili wake ameitaka
mahakama ya ICC kuahirisha kikao hicho.
Alikuwa ameamrishwa kufika mbele ya kikao hicho
cha siku mbili baada ya upande wa mashitaka
kulalamika kuwa rais huyo amekataa kuwasilisha
ushahidi mbele ya makahama hiyo.
Hata hivyo mawakili wa rais Kenyatta wameitaka
mahakama hiyo sasa kumruhusu mteja wao imma
ashiriki kikao hicho kupitia video ama skype, au
wao wajibu masuali kwa niaba yake.
Rais Kenyatta amesema kuwa yeye yuko na
shughulio n yingi sana kuweza kuhudhuria kikao
hicho mwezi ujao.
Amesema kuwa mikutano miwili muhimu ya
kiserikali ilikuwa imeshapangwa kufanyika nchini
Uganda katika tarehe hizo wanazoitisha
mahakama.
Rais huyo na naibu wake William Ruto
wanakabiliwa na mashtaka ya kupanga mauaji ya
kikabila wakati wa machafuko yaliyozuka nchini
Kenya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa
2007.
Kesi hiyo tayari imechelewehwa kwa muda mrefu
huku mashahidi wakuu wakijiondoa na pia
kumekuwa na malalamiko kuwa baadhi ya
mashahidi hao wame tolewa vitisho kubadilisha
ushahidi wao au kuondoa kabisa.
Mwendesha mashtaka mkuu Fatou Bensouda na na
mawakili wa waathiriwa wamesalia na siku tatu
sasa kujibu ombi hilo la Rais Kenyatta la
kuahhirisha kikao hicho.
Mawakili wa rais Kenyatta wame kuwa wakisisitiza
kila mara kuwa kesi hhiyo iondolewe kabisa
kutokana na kile wanachodai kuwa ukosefu wa
ushahidi dhidi yake.
Hakuna aliye shitakiwa hadi leo nchini Kenya kwa
kuhusika na kupanga machafuko hayo yaliyoizonga
Kenya mwishoni mwa mwaka wa 2007

BBC Swahili
 
You guys really expect KDF to bow down to a foreign court? i too had my beef with Uhuru but when he became CIC circumstances changed.


the only sure way to Drag Uhuru to the hague is only via a US/UK military adventure, never gonna happen in Africa.
 
Cic or not, any kenyan on a foreign court for a local crime makes me hate our focus
 
Back
Top Bottom