Super Handsome
JF-Expert Member
- Jul 16, 2013
- 3,844
- 6,448
Rais wa Marekani Donald Trump atakutana na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mjini Washington baadaye mwezi huu, kujadili masuala ya usalama na biashara.
Hayo yametangazwa na Ikulu ya Marekani White House jana-Jumatatu. Kwenye taarifa, White House imesema, Kenya ni mshirika muhimu kwa Marekani, na Rais Trump anatazamia kujadili masuala ya kutanua mikakati ya ushirikiano kulingana na maadili ya kidemokrasia na masilahi ya nchi hizo mbili. Taarifa hiyo imeleza zaidi kuwa Rais Trump na Rais Kenyatta watajadili njia za kuimarisha biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo mbili huku wakiimarisha ushirikiano wa kiusalama.
Rais Kenyatta anatarajiwa kuzuru Marekani Agosti 27. Atakuwa rais wa tatu kutoka Afrika kuzuru White House chini ya utawala wa Trump baada ya rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi kuzuru mwaka uliopita, na rais wa Nigeria Muhammadu Buhari kuzuru Aprili mwaka huu.
NB ; Hili zigo letu halina mpango! fursa kama hizi ye hajui ..anajua kugawa mapapai tu! shame on us!