Watu hao walijumuisha vijana, wahitimu wa vyuo vikuu na watu wenye taaluma mbalimbali. Baadhi walifika mapema alfajiri wakitumaini kupata nafasi ya kuajiriwa.
Tukio hilo limeibua maswali kuhusu idadi ya nafasi zilizokuwepo, ushindani katika soko la ajira na changamoto zinazowakabili Wakenya wanaotafuta kazi.
Je, tatizo kuu la ajira Kenya ni ukosefu wa nafasi za kazi, kutolingana kwa ujuzi na mahitaji ya soko, au mfumo wa uchumi ambao hautengenezi ajira kwa kasi inayohitajika?
Na je, Serikali, sekta binafsi na viongozi wa kisiasa wanapaswa kuwajibika vipi katika kutafuta suluhu?