Joss
JF-Expert Member
- May 28, 2009
- 765
- 191
Kuna hii baa ya La Patrona, karibu na kanisa la Katoliki, Nkuhungu, Dodoma. Iko vizuri kimazingira ila inatupa kero wakazi wa jirani. Inapiga mziki mnene kila siku kuanzia mida ya saa nne hivi hadi saa kumi hivi usiku, tena yupo na DJ anapiga kelele mno.
Kuna uzi uliletwa siku chache zilizopita ikizitaja na baa zingine za jirani kupiga mziki usiku kucha.
Baa zilizopo jirani na Kanisa Katoliki Nkuhungu ni kero kwa kupiga muziki usiku mzima
Hizi baa zingine za Stela na Revola wamejirekebisha, nilipofatilia nikagundua kuwa walisoma ule uzi. Sasa hii ya La Patrona bado wanapiga kama kawaida.
Sasa hivi mziki inapigwa, niko kama mita 300 kutoka hapo ila mziki ni kama uko chumba cha pili. Sisi wakazi tunaumia, usiku ni muda wa kupumzika. Tafadhali vyombo husika mtusaidie. Malalamiko yetu hayafanyiwi kazi.