Kero hii ya kutofikishwa kileleni

Kero hii ya kutofikishwa kileleni

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Unapoona kwenye mahusiano watu wanagombana lakini hawaachani jua hao wanapendana sana na hutimiziana haja zao mubashara kabisa! Hufikishana kileleni!!!

Mahusiano mengi yamevunjika kutokana na tatizo sugu la kutofikishana kileleni hakika hii ni Kero kubwa mno
Elimu ina pande mbili, unaweza kusoma na ukafaulu mitihani lakini usielimike na mwingine anaweza asisome elimu rasmi lakini akaelimika na kuwa mtu bora kabisa

Ni katika hilo la elimu kuna utashi utayari kujituma kuelewa na kiwango cha IQ pia! Kuna watu kwa njia za ajabu kabisa wamepata mafanikio yanayoliliwa na wengi lakini kwakuwa kiwango chao cha ufahamu ni kidogo sana wamejikuta wanaangukia pua na kufeli kabisa

Kwenye mfumo wa taa za magari kuna taa inawaka sana inaitwa spotlight...hii haiwashwi hovyo! Dar es salaam ni spotlight ya nchi kuna tofauti kubwa sana kati ya rc wa Kigoma na rc wa Dar

Chochote kinachofanywa Dar kinakuwa kama mwongozo wa kwingine kote
Mtu ambaye anabamba sana kwasasa kwenye mijadala ni bwana Makonda (bashite?) vyovyote iwavyo kati ya wengi wanaomponda wengine ni kutokana tu na wivu na kijicho! U-rc wa Dar si nafasi ndogo ati pesa hata kama huitaki itakufuata tu na ukiikataa basi unahitaji kupimwa akili

Tumjadili rc kwa hulka yake ya kutotimiza yale anayoyaanzisha. Hili halina tofauti na ile Kero ya kutofikishwa kileleni
Hulka hii mbaya ni sawa na chumba kile cha mahututi gereza la fikra
Haya yameishia wapi?

Vitambulisho maalum vya walimu ili wapande bure
Dar tuitakayo
Operation Ondoa ombaomba
Kero za wanadarisalama
Na operation nyingine nyingi zilizifeli kabisa

Shida ni moja maandalizi na kushirikishana hakuna. Lakini Dar ni jiji lenye wataalam na wasomi wa kila kaliba iweje hakuna kujadiliana kwanza?
La dawa za kulevya ndio bye-bye tumeachwa na hamu zetu hatujafikishwa kileleni tunachafuliwa tu kila wakati

Kama ukiamua kuwa banditu baki hivyohivyo usiwe kama mkate mgumu mbele ya chai
Mwanaume kakaa mahabusu siku zaidi ya 100 lakini katoka na tabasamu wewe Leo kuombwa tu kuonyesha vyeti unamwaga michozi hadharani! Nini maana ya kuwa kiongozi?
 
Mwanzo nilijua hii mada itawagusa zaidi wanaume wa Dar, lakini nilivyozidi kushuka niliongeza umakini katika kusoma na kutafakari. Hii ni hoja nzito Mkuu wangu.

RC anachofanya ni kugusa, anajifanya kung'ata kisha kupuliza na baadae kupotezea huku mwanzoni akibeba sifa lukuki.

By the way, Mkuu mshana jr unatumia simu gani? Hahaha.... ( INFINIX-X551)
 
Kama anashindwa kushirikiana na wenzake na kuwafikisha wenzake kileleni ina maana hana nguvu za kutosha
Huyu ni msanii underground anayetafuta single ya kutokea, kila Mara anatupia singles bahati mbaya hizo single zinashindwa Ku hit
 
Mwanzo nilijua hii mada itawagusa zaidi wanaume wa Dar, lakini nilivyozidi kushuka niliongeza umakini katika kusoma na kutafakari. Hii ni hoja nzito Mkuu wangu.

RC anachofanya ni kugusa, anajifanya kung'ata kisha kupuliza na baadae kupotezea huku mwanzoni akibeba sifa lukuki.

By the way, Mkuu mshana jr unatumia simu gani? Hahaha.... ( INFINIX-X551)
[emoji111] [emoji817] [emoji3] google tu utaiona

Sent from my INFINIX-X551 using JamiiForums mobile app
 
Dah, wewe Mshana ni Noma, huu utakimbiliwa na wapenda ngono zaidi, hii itatoa uhuru wa mawazo. Kuliko heading ingekua " Rc..... Hajawahi kutufikisha kileleni". Hapo lingekuja povu la ajabu sana.
[emoji23][emoji23][emoji23] wapenda ngono tumekuja tunakutana na intelligensia ya ajabu!!! Mkuu kapangilia hoja yake vizuri sana
 
[emoji23][emoji23][emoji23] wapenda ngono tumekuja tunakutana na intelligensia ya ajabu!!! Mkuu kapangilia hoja yake vizuri sana
Ha ha ha haaa.. Me mwenyewe nilikuja kingono ngono.. Mshana ni mjanja sana, huu ni uzi wake wa pili nausoma ukiangalia juu juu utafikiri ni uzi wa kwenye jukwaa la Mambo ya Kikubwa. KUUUUMBE.
 
Ha ha ha haaa.. Me mwenyewe nilikuja kingono ngono.. Mshana ni mjanja sana, huu ni uzi wake wa pili nausoma ukiangalia juu juu utafikiri ni uzi wa kwenye jukwaa la Mambo ya Kikubwa. KUUUUMBE.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ana akili ya kiuandishi!
Sio wengine hapa kujua kusoma na kuandika tunajifanya waandishi na kuleta mada zisizo na kiuno.
 
Back
Top Bottom