Kero ja ujenzi Jiji zima la Dar esalaam

Kero ja ujenzi Jiji zima la Dar esalaam

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
Kwa sasa hivi na muda huu kuna miradi ya barabara inatekelezwa na wachina jiji zima la Dar es salaam.
Niitaje:
-Airport -KAMATA/Aggrey st.
-Bibi Titi Rd
-Ali Hassan Mwinyi rd
-Morrocco-Mwenge rd
-Ubungo-Kimara rd
-Ubungo -Mwenge rd
-Mwenge-Tegeta/Basihaya rd
-Kawawa /Msimbazi
-Azikiwe /Posta Mpya rd

Tunajua kuwa haya ni maboresho makubwa ya Jiji la Dar es salaam, lakini sasa kero ya kuingia Jiji la DSM na kutoka ni kubwa mno.
Uongozaji wa magari(Traffic Management) na utengenezaji wa njia mbadala(Diversions) ni kama haupo kabisa.
Wachina wanapuyanga kama wanavyojua wao.
 
Yan folen ya jmos sitoweza kusahau,,, si Shanghai wazungu wakiipenda zenj kuliko huku,,, foleni ya bongo🙌🏽sasa usiombe mvua inyeshe
 
Vurugu tupu nawaonea wenye magari

Ova
 
Kweli wewe ni wale kina njomba nchumali, kukijengwa nchale, kusipojengwa nchale, zikiliwa zote nchale, zikifanya kazi nchale... Mama anatakiwa achimung'unye wala achiteme...
 
Sijawahi kuona nchi yenye watu wasiojali maisha yao km watanzania..haihitaji kuambiwa shida kubwa zinazoweza kuwepo unapobomoa barabara nyingi kwa wakati mmoja na matengenezo yanafanyika mchana tu..lkn barabarani kuna watoto, wagonjwa, wazee, walemavu wanaohitaji kufika haraka wanakokwenda..siioni sababu za kubomoa barabara zote hizo kwa pamoja badala ya kuweka awamu kulingana na muunganiko wake ili kupunguza kero ya foleni..! Tanzania Kila mahali unaona ubinafsi na wizi!
 
Kwa sasa hivi na muda huu kuna miradi ya barabara inatekelezwa na wachina jiji zima la Dar es salaam.
Niitaje:
-Airport -KAMATA/Aggrey st.
-Bibi Titi Rd
-Ali Hassan Mwinyi rd
-Morrocco-Mwenge rd
-Ubungo-Kimara rd
-Ubungo -Mwenge rd
-Mwenge-Tegeta/Basihaya rd
-Kawawa /Msimbazi
-Azikiwe /Posta Mpya rd

Tunajua kuwa haya ni maboresho makubwa ya Jiji la Dar es salaam, lakini sasa kero ya kuingia Jiji la DSM na kutoka ni kubwa mno.
Uongozaji wa magari(Traffic Management) na utengenezaji wa njia mbadala(Diversions) ni kama haupo kabisa.
Wachina wanapuyanga kama wanavyojua wao.
Ndio utawala wa huyo mama huo.
 
Sijawahi kuona nchi yenye watu wasiojali maisha yao km watanzania..haihitaji kuambiwa shida kubwa zinazoweza kuwepo unapobomoa barabara nyingi kwa wakati mmoja na matengenezo yanafanyika mchana tu..lkn barabarani kuna watoto, wagonjwa, wazee, walemavu wanaohitaji kufika haraka wanakokwenda..siioni sababu za kubomoa barabara zote hizo kwa pamoja badala ya kuweka awamu kulingana na muunganiko wake ili kupunguza kero ya foleni..! Tanzania Kila mahali unaona ubinafsi na wizi!
Ujenzi wa kuhalalisha matumizi ya heLa za Uma na upigaji.
Bora zingejengwa barabara za mzunguko (ring roads) kuliko kinachoitwa mwendokasi katikati ya jiji. Mipango miji ni changamoto.
 
Kweli wewe ni wale kina njomba nchumali, kukijengwa nchale, kusipojengwa nchale, zikiliwa zote nchale, zikifanya kazi nchale... Mama anatakiwa achimung'unye wala achiteme...
Tazama kwa jicho la tstu vile vile
 
Ki ukweli kila mwenye akili ana question ni maamuzi ya waziri wa ujenzi au baraza zima la mawaziri dsm yote kuchimbuliwa vijibarabara vinavyojengwa vyembamba vidogo na hicho kimwendokasi kimoja kisicho mabasi.

Tungeiga jiji kama Abdjan na Ivory cost kwa ujumla kuhusu barabara ingependeza sana. Au hata Tunis maana tukisema Cairo tutajidanganya.

Hivi hatuna wasomi wanaopenda maendeleo ya kweli kuliko hili la bora liende.

Mfano kigamboni sasa lami mpya zimebanduliwa nadhani watajenga upya bila kupanua barabara na kupitisha mfumo wa maji taka.
 
Back
Top Bottom