Kero kero kero!

Kero kero kero!

Tatizo sio matendo kana kwamba utaendelea kununiwa ila kusahau kunashindikana kwahiyo ukirudia tena unakumbushiwa!

Unapoombwa samahani haina maana kwamba usahau yaliyotokea basi umsamehe na kuanza mstari mpya. Sasa likitokea kosa jingine ukakumbushia na lile kosa la mwaka 47 ambalo mkosaji alishasamehewa hapo ndipo kasheshe inapoanzia.
 
Kwahiyo hua mnaumia kukumbushwa mlivyokua wabaya..wakorofi au waongo back in 1947?
 
Hapo Bishanga umeongea kweli kabisa.
Sisi wanawake tunazo hizo tabia na mimi nakiri na ninaoba wanawake wenzangu tujirekebishe ili kunusuru mahusiano yetu. ILA SASA HAPA JF BADALA YA WADADA KUCHANGIA UTASIKIA WANA COMMENT SIYO WANAWAKE WOTE. NYIE KILA KITU KIBAYA MNAKUWA NDO TOFAUTI NA WANAWAKE WENGINE. TOENI COMMENT NINI KINATUFANYA TUWE HIVYO AND NOT CHEAP TALKS LIKE SIYO WOTE. I HATE THOSE FLUFFY TALKS
 
Kwahiyo hua mnaumia kukumbushwa mlivyokua wabaya..wakorofi au waongo back in 1947?

Mhhhh! Binadamu hatuko perfect Lizzy...makosa yanatendwa na jinsia zote sasa unapoombwa samahani na kuikubali samahani hiyo haina maana kuanzia hapo mtu atakuwa perfect na kutotenda kosa lingine, sasa ugomvi wa kosa lililotendwa leo hii ni tofauti sana na ugomvi ambao umejumuisha makosa yote ya tangu mwaka 47 hadi leo hii.
 
acha nikakugongee senks bishanga. lembea madongo mwanawane , ndio zao hawa! na wakiendelea tutawataja kwa majina. na mimi nina hasira flani hivi
 
Mhhhh! Binadamu hatuko perfect Lizzy...makosa yanatendwa na jinsia zote sasa unapoombwa samahani na kuikubali samahani hiyo haina maana kuanzia hapo mtu atakuwa perfect na kutotenda kosa lingine, sasa ugomvi wa kosa lililotendwa leo hii ni tofauti sana na ugomvi ambao umejumuisha makosa yote ya tangu mwaka 47 hadi leo hii.

Kama ambavyo wewe hauko perfect ndivyo na kwangu pia!Kama wewe bado unaendelea kukosea kwanini kukumbushia kwangu ndio kuwe tabu?
 
Very true wanawake tuna maudhi bana. Ushauri kwenu kaka zangu muwe makini mnapotutafuta kuna wengi wa wanawake ni tegemezi kupita maelezo.
 
Kila kukicha kinamama wana MMU kazi kutusimanga,sasa leo na mimi ngoja niwatolee uvivu.Kinamama mnatukera kwa haya yafuatayo:
1.Utegemezi: Unambeep mmeo/hawara/bf,nini mama?unamuuliza, 'naomba unitumie vocha',sawa nakurushia ya elfu kumi,muda mchache baadae unanibeep,nakupigia 'luku imeisha baba'sasa nambieni hiyo vocha elfu kumi huwa mnampigia nani? au ni kwa ajili ya kupigia umbea,'Eh mwenzangu jana si nikamwona Bishanga anaingia gest',inahusu?
2.Wivu: Mara upekenyue simu yangu,nikirudi nyumbani 'oh ulikuwa wapi' mara 'nani huyo ulimpakia kwenye gari',nikivua nguo mara unuse kufuli langu, jamani ya nini yote haya? mbona sisi hatuwafatilii hivyo?
3.Kununa: Mara unune,mara uvimbe,mara unisonye kwa mbali,nimekukosea nini? nikuuliza husemi kitu,mkoje jamani?
4. Gubu:Hata kama nilikukosea mwaka 1947 na nikakuomba radhi ukajitia umenisamehe ni bure tu,nikikukosea kidogo leo ,utasikia 'oh ndo mana nilikubamba na hausgel'sasa jamani tukio la 1970 unalibebea bango mpaka leo,we umenikosea mangapi mbona huwa sirudii kuyakumbushia?
5.Mnaongea mno: Wanawake mnaongea jamani, pich pich pich pich,du,hamchoki mkaacha na waume/hawara/bf zenu wakaongea?
6.Uvivu: Sasa kuajiri housegirl ndo iwe sababu ya huyo housegirl kufua hadi kufuli zangu,na kibaya zaidi baba akiumwa eti yeye ndo anamkumbusha dawa,chakula anampakulia yeye,halafu mzee akimfanzia mnakuja juu.
7.Ubinafsi: Nikilipa schoolfees za mdogo wako poa tu,paa la nyumba ya shangazi yako likiepuliwa na kimbunga nikatoa pesa ya mabati poa tu,mama yako akiumwa nikampeleka India poa tu,lakini shuhudia mtoto wa dada yangu akose karo nimlipie au nimnunulie ka gari baba yangu mstahafu,huo mziki wake utaukoma,'eh ndo mana hatuendelei sijui nini sijui nini' lol!
Ngoja nipumzike kwanza ntarudi baadae,nina hasira flan hivi.

lol, yamekukuta mwenzangu! Pole.

Kibaya zaidi hizi tabia atarithishwa binti yako (kama umezaa na mwanamke aina hii).
 
Back
Top Bottom