KERO Kero kuhusu maji machafu katika eneo la Michungwani Darajani, Kimara

KERO Kero kuhusu maji machafu katika eneo la Michungwani Darajani, Kimara

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mmoja wa wakazi wa Kimara, naomba msaada wenu kufichua changamoto ya maji machafu yanayotolewa na DAWASA katika eneo la Michungwani Darajani.

Maji haya yamekuwa yakisababisha baadhi ya wananchi kupata matatizo ya ngozi, ikiwemo kuwashwa na mzio (aleji) baada ya kuyatumia.

Naomba mamlaka husika zifanye uchunguzi wa haraka kubaini chanzo cha tatizo hili na kuchukua hatua stahiki ili wananchi wapate maji safi na salama kwa matumizi ya kila siku.

Tunatumaini suala hili litafanyiwa kazi kwa uzito unaostahili, kwani wananchi wanahitaji zaidi ya kulipishwa bili za maji; wanahitaji pia huduma yenye ubora na usalama.
 
Back
Top Bottom