KERO Kero kuhusu ufadhili wa masomo kwa watumishi wa afya kupitia mradi wa Beginning Fund mwaka wa fedha 2026/2027

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kuna barua inayosambaa kutoka Wizara ya Afya ikionesha uwepo wa ufadhili wa masomo kwa watumishi wenye Diploma kupitia mradi wa Beginning Fund kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Cha kusikitisha ni kwamba kwa upande wa wauguzi, ufadhili huo umeelekezwa zaidi kwenye ngazi ya Higher Diploma, ambayo haipo kwenye muundo wa utumishi wa kada ya uuguzi.

Aidha, baadhi ya fani zilizotajwa ni:
  1. Anaesthetic Nursing – Kwa uhalisia hakuna chuo Tanzania kinachotoa kozi hii kwa ngazi ya Higher Diploma. Vyuo vingi vinatoa short course ya mwaka mmoja, mfano Bugando na Benjamin Mkapa. Kwa mujibu wa Msajili wa Baraza la Uuguzi, Bi. Agness Mtawa, kozi hiyo hutambulika kama CPD.
  2. Operating Theatre Management
  3. Midwifery
Swali letu kwa Wizara ya Afya ni kwa nini ufadhili huu usielekezwe kwenye ngazi ya Shahada kama ilivyofanyika kwa kozi nyingine kama Biomedical Engineering, wakati kuna shahada za Nursing Anaesthesia na Midwifery zinazotolewa na MUHAS badala ya Higher Diploma ambazo hazipo kwenye muundo wa uuguzi.

Hatupingi ufadhili huu kwa kuwa unalenga kuboresha taaluma na ujuzi katika utoaji wa huduma kwa wananchi. Hata hivyo, tunaomba Wizara itoe ufafanuzi kuhusu kozi za Higher Diploma zinazolengwa na ituambie ni vyuo gani Tanzania vinatoa kozi hizo, kwani hata kwenye mwongozo wa udahili wa NACTVET wa mwaka wa masomo 2026/2027 hazijaonekana.

Wauguzi tunasikitishwa na changamoto za muundo wa kada yetu. Mtu anaposoma kozi ambayo haipo kwenye muundo wa utumishi, inalenga nini hasa?

Tunaomba Serikali ilitazame suala hili kwa kina na irejee muundo mpya wa kada ya uuguzi uliopendekezwa mwaka 2023, ili ufadhili utolewe kulingana na ngazi husika za taaluma.

Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mwigulu Nchemba, tunaomba uingilie kati suala hili. Kwa uhalisia, wanaoumia zaidi ni watumishi wa ngazi za chini.

Tunaomba maboresho yaliyofanyika yaanze kutekelezwa, kwani tumechoka na ahadi za kila mwaka.

Nawasilisha.
 
Attachments

Pole sana,

Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mwigulu Nchemba, tunaomba uingilie kati suala hili.
Suala hili liko chini ya wizara ya afya yenye waziri wake, sasa kwa nini huyo waziri asiingilie kati yeye badala ya waziri mkuu? Nafikiri waziri wa wizara husika ndiyo aingilie kati.

Pia kwenye barua ya tangazo (uliloambatanisha hapo juu) kuna namba na email iliyotolewa kwa ajili ya maelezo zaidi kuhusu tangazo husika. Sasa kwa nini usingetumia hiyo namba au email kuwafikia wahusika kwa haraka ili watoe ufafanuzi kuhusu haya malalamiko yako? 👇

1784118415299.jpg

Kila la kheri.
 
Back
Top Bottom