KERO: Masanja Mkandamizaji kutumia Ulokole kinyume na maadili ya Kipentekoste

KERO: Masanja Mkandamizaji kutumia Ulokole kinyume na maadili ya Kipentekoste

Biblia imetoa mwongozo wa mavazi kwa wakiristo wore.
Huwezi vaa vibaya ukasema sio tatizo eti kwakuwa una moyo safi
Ni sawa upewe mahubiri na shetani useme eti nafuata maneno yake sijali matendo yake.shetani atabaki kuwa shetani na kamwe hawezi mtukuza Mungu.
Tupe andiko.,.
 
Umeongea kweli na hakika,MTU anabaki kuacha kuabudu eti kisa Fulani kamkwaza,kumbe hajui kuwa anajichelewesha safari ya mbinguni,big up,ujumbe huu ni hakika na ndivyo ilivyo..barikiwa sana kwa kumtetea Yesu na kuitetea injili
Unaabudu kwa kuangalia na sehemu unakoabudu. Utaonaje mtu ni tapeli kabisa halafu wewe ukimbilie kusalishwa naye? Ulokole siku hizi umekuwa kichaka cha uasherati na usinzi!
 
Wajinga waliwao....kwa kweli nashindwa kuelewa hivi kwanini mtu ama watu wanashindwa kujifanyia vitu vyao mpaka waone celebrity fulani kafanya? Ujinga huu ndio unawafanya watu/jamii za kiafrika kuwa watumwa wa dini za watu....this is stupid. Uislam na Ukristu si dini zetu, waachieni wenye nazo waziendekeze.
 
Biblia imetoa mwongozo wa mavazi kwa wakiristo wore.
Huwezi vaa vibaya ukasema sio tatizo eti kwakuwa una moyo safi
Ni sawa upewe mahubiri na shetani useme eti nafuata maneno yake sijali matendo yake.shetani atabaki kuwa shetani na kamwe hawezi mtukuza Mungu.
je umetoa kuna muongozo wa mavazi kwa walokoke ?
 
Habari ya mda Huu..

Asilimia kubwa ya watu duniani wanaamini uwepo wa Mungu, na uwepo huu wa Mungu umeleta Imani tofauti tofauti za ambazo binadamu huziishi. Na Imani hizi zinaheshimiwa, wapo wenzetu waroma, wakatholiki, wapentekoste, kila imani inataratibu zake na miiko yake inayoheshimiwa na kila muumini wa dini hiyo.


Kwa upande wa wapentekoste, sote twajua namna miiko yao ilivyo hasa katika mavazi, tumeona kwa waroma tumeona kwa waanglikana, zaidi sana hata kwa wenzetu waislamu.Uwepo wa dini hizi umekuwa msaada sana kwa jamii hasa kuibadilisha jamii na hasa vijana kuwa na miiko na heshima.

Lakini siku za hivi karibuni, kumekuwepo na wimbi la vijana wanaokimbilia ulokole lakini matendo yao hayaendani na miiko ya kilokole, bika kupepesa pepesa kumekuwa na celebrity huyu anayefahamika kama "Massanja mkandamizaji" ama "Emmanuel Mgaya" huyu amekuwa akijiita PASTOR.

Kumekuwa na malalamiko mengi hasa toka wa vijana wakilokole wakilalamika mienendo ya celebrity huyu na mavazi yake yasiyoendana na miiko ya kilokole, ki ukweki kuna wakati ukimwona ni kama kijana mwingine tu wa mitaani, kuvaa mlegezo, kusuka nywele, kofia kuvalia nyuma, hivi haviendani na miiko ya kikristo.

Kwenye jamii inaonyesha picha kuwa Anajifichia kwenye mwamvuli wa kipentekoste ili hali si mpentekoste...sasa unamdanganya nani massanja? hata moyo wako ukushuhudie kuwa.

Unachokifanya hakiendani na maadili ya kipentekoste, kumbuka wewe ni kioo na ni maarufu, hivyo either ubadili namna unavyovaa au uache kutumia ulokole kama kivuli cha maovu!

HAPO ALIKUWA ANAKUNYWA ULANZI
[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]

"massanja mkandamizaji" kujiita ameokoka tena mchungaji mtarajiwa!!!

[emoji115][emoji115][emoji115][emoji115][emoji115][emoji115][emoji115][emoji115][emoji115][emoji115][emoji115][emoji115]

Unaharibu Taratibu za kipentekoste!


Ujumbe huu ukufikie mahali pote ulipo
92395f03f88a62a17fe2ae4374070d17.jpg

u
Acheni mawazo mgando,mambo mengi kwenye hizi Dini zetu yameingia,hayakuwepo hata enzi za Jesus,
Makanisani mnaimba sembene,mnakata mauno,tuonyesheni wapi,katika bible Jesus au manabii wengine,walipiga magitaa na kucheza sebene kanisani,
Hayo mavazi ambayo wewe unaona ni kikwazo,kwa "upentekoste wa kibongo" unayaangaria kwa jicho la kiutamaduni zaidi,
Kwa America ni mavazi ya kawaida,
Kama Mungu ni mmoja,kwa nini asimuhukumu Mmarekani akivaa hivyo,lakini amuhukumu Mtz akivaa mavazi ya Tamaduni zingine,
Ucha Mungu haufungwi na mipaka ya Tamaduni,
 
Tatizo haliko kwenye mavazi anayovaa, tatizo ni tabia ya kujionesha na kujisifu sana kama watu waovu wafanyavyo. Massanja hana tofauti na watu wenye kushinda na kujionesha kwenye mitandao ya kijamii nguo wanazovaa na chakula wanachokula.

Mkristo wa kweli, mwenye kuiujua KWELI hawezi kuwa mfano wa kujionesha na kujisifu na kujikweza kama Masanja. Matendo yake yanadhahirisha kuwa Masanja siyo Mkristo wa kweli achilia mbali kuwa Pastor au Mchungaji, huyu ni mganga njaa tu kama wengine.
 
Mfanyabiashara
Nimelipenda sana hilo jibu; "Mfanyabiashara"..ni kweli kabisa, Masanja ni mfanyabiashara anayetafuta "followers" wengi kwenye Instagram page kama wafanyavyo akina Sanchi, Wema Sepetu, Idrisa Sultan n.k. Masanja siyo Mchungaji wala hana sifa za kuwa mchungaji, huyu ni kondoo aliyepotea.
 
Ukikariri saaaaana mwisho unachanganyikiwa chukulia kila kitu kwa wepesi, binafsi ndani ya imani yangu na maisha ya ujana kwa ujumla sioni tatizo kwa MASANJA MKANDAMIZAJI.

Aliwahi kuja hapa nchini REBECCA MALOPE akiwa amevaa pensi fupi, kama kawaida waandishi wetu waliozoea kukosoana kiimani kupitia mavazi.walimuuluza jibu lake lilikuwa fupi, imani ya MTU iko rohoni mwake.

Niliwahi pia kumsikiliza EVANDER HOLLYFIELD bondia mahiri kwa enzi zake, pale alipogundulika na tundu katika Moyo wake na kuzuiwa kupigana aliamua kwenda kwa mchungaji kuombewa.

Mchungaji alimuuliza nn? Kilichomfanya aende kwake kuombewa! Akajibu kuwa alimuomba Mungu kw a kusema yy ndiye aliyempa Uwezo ule wa kupigana na kupata kipato kupitia mchezo wa gumi.

Sasa anaumwa hawezi tena kucheza mchezo ule, ndipo akaona amfuate mchungaji kwa maombi zaidi.

Aliombewa na kupona akarudi ulingoni na kupambana na TYSON na kumshinda.

Nilimuuliza mlokole mmoja je? Mchezo wa ngumi walokole mnauchukuliaje? Alijibu ni dhambi kabisa. ( kwangu napata fundisho pia dini na tamaduni wakati mwingine zinakwenda pamoja)

Kuna wimbi la vijana duniani kufanana kutokana na dunia sasa kuwa ni kijiji, haizuii mavazi kufanana, chakula ,lafudhi na mambo kedekede.

Kikubwa mambo hayo yanawaelekeza katika dhambi? Au yanazidisha UPAKO vijana wanavutika wanazidi kumpenda BWANA NA MWOKOZI WAO. Hawaishi tena katika sheria Bali kwa neno lile liletalo uzima.

Vifungo vyooote vilifunguliwa pale msalabani.
 
Back
Top Bottom