Kero nilizokutana nazo Dar natamani kurudi mkoani

Muzine

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2017
Posts
32,366
Reaction score
60,453
Habar wana JF
Bora tu makao makuu yahamie Dodoma sioni raha ya kubaki Dar .
Jana naingia dar nakaribishwa na mvua
Umeme hakuna
Joto balaa
Watu wa Dar karibuni mkoani mpate raha Kwanza sisi Umeme unapatikana masaa 24.
Alafu foleni yani unatembea Kimara hadi Masaki masaa 5 kuna raha gani.
Ndo maana mkulu anataka kuhamia Dodoma sio Kwa Kero hizi.

Ila Dar kuzuri tatizo Kero zake tu ndo zinakatisha tamaa.
 
Mkulu anahamia dodoma kwa yake. Maana yeye anaishi pembeni ya bahari. Foleni hazimuhusu maana muda wowote atakao pita barabara inakua nyeupe anapita prke yake
 
Dar kutamu asikwambie mtu. Pamoja na dhiki zote watu hawahami. Ukizoea zoea hutotamani kuondoka. Leo wk end njoo nikakupe bata za kufa mtu ili upate kitu cha kukumbukia Dar!
Nikahadithie mkoani uzur wa Dar na Kero zake
 
Kama si mzoefu wa dar ukikaa week unaweza kuisi uko kifungoni.

Dar kuna kero nyingi lile jiji kuna haja ya kulipanua kweli kweli
Nashukuru mkulu anasema wahamie Dodoma kupunguza jam na waendelee tu kubomoa Kiukweli maana hakuna hewa kabisa japo ni pazuri
 
Mkulu anahamia dodoma kwa yake. Maana yeye anaishi pembeni ya bahari. Foleni hazimuhusu maana muda wowote atakao pita barabara inakua nyeupe anapita prke yake
Anatuonea huruma wa mkoani tukija Dar
 
Nashukuru mkulu anasema wahamie Dodoma kupunguza jam na waendelee tu kubomoa Kiukweli maana hakuna hewa kabisa japo ni pazuri



Ha ha ha kwani kutokuwepo kwa hewa kunasababishwa na majengo? Miji na majiji yaliokaribu na bahari joto lake si mchezo. Mombasa. Tanga.
 
Yeah! Na shughuli pevu ya wanaume wa Dar! Si mikoani mnasema wanaume wa Dar wameathirika na kiepe yai!
Bora umenikumbusha jana nimepata maeneo nikakuta wanaume kama 7 wanakula chips kidar na soda mm nkmefika nikaagiza ugali Tena upo Kama ngumi nilimwambia mhudumu ongeza na mwingne watu wote wakanishangaa nikanunua na Coca ya moto nikashushia sitak kuumwa koo na vitu vya baridi nikachukua na maji ya seque kubwa nikashushia macho yote kwangu
 
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ Weye noma. Sasa leo twende ukale Pizza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…