Kelela
Senior Member
- Nov 7, 2020
- 191
- 308
Habari wana JF,
Naandika uzi huu ili kuelezea kero zangu na wengine wengi kuhusu RITA kama kuna wahusika humu walifanyie kazi.
Natoa kero hizi leo Tarehe 26-Julai-2022
1. Kero ya Kwanza: Namba ya Huduma kwa wateja ni BUTU.
Namba ya Huduma kwa wateja ya RITA haifanyi kazi, yaani ukipiga inaongea matangazo kidogo, ikifika sekunde ya 30 inajikata wenyewe. Tumeshalalamika hili katika social media zao lakini hakuna matokeo.
2. Kero ya Pili: Uchelewaji wa Kupata Cheti cha Kuzaliwa (Online Registration).
Kwa kawaida ilikuw ukiapply cheti cha kuzaliwa mtandaoni inaweza kuchukua wiki 1 hadi 2 au imezidi 3 unapata cheti chako, lakini sasa hivi unaweza kukaa hata miezi miwili na bado haujapata, unaweza kwenda ofisini kwao hata mara 5 au 6 kwa ahadi unazopewa na kila ukienda unapigwa kalenda. Na tatizo hili lipo hata katika kuhakiki vyeti vya kuzaliwa na vifo inachelewa sana siku hizi.
3. Kero ya Tatu: Changamoto ya mfumo.
Changamoto hii ipo kwenye ku-upload attachments, kama umekosea ku-upload attachment tofauti ndio basi tena hauwezi kuiondoa. Ingawa kuna option ya Remove, Lakini ukibonyeza Remove inakuletea ujumbe kuwa Error Occured.
Kama mupo wahusika humu wa RITA wayafanyie kazi hayo, watu wanahangaika, Kwa anayetaka ushahidi wa haya niliyoandika, Ingia Page ya RITA Tanzania Facebook Kisha angalia sehemu ya comments uone watu wanavyolalamika.
Wa salam!