Kero soko la mitumba Karume

Kero soko la mitumba Karume

MKUU,

KWA KUKUSAIDIA,
NAMNA RAHISI YA KUNUNUA BIDHAA KWA WAMACHINGA WA KARUME IKO HIVI ;

BEI WATAKAYOKUTAJIA,
ONDOA ILE SIFURI YA MWISHO WAKATI WA KUBERGAIN,

UKIAMBIWA BIDHAA NI SH. 80,000/=,
WAAMBIE NINA ELFU NANE AU HATA ELFU NNE-

USIONE AIBU KUWASHUSHA MAANA'KE WAO HAWAKUONEI AIBU WANAPOKUDUFUA LAKI MOJA KWA SHATI LA BUKU JERO.
 
watakula wapi?, hiyo sio juu ya mteja, wao waache uhuni, wanaharibu sifa ya soko wapumbavu sana
Karume madalali ni wengi kuliko wenye biashara. Madalali wanaanza kukufatilia pale unapoingia sokoni Mara braza mashati,viatu,mabegi sijui nini na nini. Wanakera sana, mi nawaambiaga natafuta taulo za buku buku hapo huwa wanageuza wenyewe[emoji4] [emoji4]
 
Karume madalali ni wengi kuliko wenye biashara. Madalali wanaanza kukufatilia pale unapoingia sokoni Mara braza mashati,viatu,mabegi sijui nini na nini. Wanakera sana, mi nawaambiaga natafuta taulo za buku buku hapo huwa wanageuza wenyewe[emoji4] [emoji4]
hahah
 
Habarini wadau.

Kuna kitu huwa kinanitokea kila ninapokwenda soko la Karume Dar Es salaam.
Nimekuwa nikienda kununua nguo, viatu na mabegi kwa muda mrefu tu.... kero inakuja pale unapokuwa unachagua bidhaa yeyote tajwa hapo juu wahuni/madalali/wapiga debe wanakuja wanaanza kukuchagulia kwa nguvu kuhu wanaweza hata kukupatia kiatu cha kike & wakakusifia umependeza...... issue ni pale utapoghahiri usinunue wanaweza kukuzingua, pia utakapoa amua kukunua wataanza bei ya juu sana kwa kuweka cha juu.

Mfano: leo baada ya miangaiko yangu ya siku, niliamua kwenda karume kutafuta kiatu cha mitumba cha kawaida tu.... hao wahuni walikuja kama 4 wakaanza kunisaidia kuchagua, nikafanikiwa kupata kiatu, nikauliza bei wakaanza 65,000, sikubishana nao sana maana nilikuwa serious nimenuna nikawaambia chukueni 20,000 kama hawatakia basi. Wakaanza kunizingua nikawapiga mkwara mzito sana... wakanieshimu ghafla wakachukua hizo pesa kiroho safi tu.

Issue ni hao wahuni wanaoingilia biashara za watu na kuvuruga wateja ni kero sana....

Hadi nimejisemea moyoni siendi tena karume kununua kitu.... bora niende manzese au soko jingine.

Unaweza kuuziwa kitu cha 10,000 kwa bei ya 45,000.

Pia na wafanya biashara wajitahidi waache kuruhusu hawa watu kuweka chajuu sana.
Siku nyingine ukifika karume waambie umeenda kushangaa totozi wa mjini,waambie wakuonyeshe watoto wazuri wapo sehemu gani![emoji23]
 
Back
Top Bottom