Kero tunazokutana nazo kwenye vibanda umiza

Kero ingine ni pale unapokaa karibu na mtu mwenye midadi. Mpaka mpira uishe unaweza kutoka na ngeo na manundu ya kutosha.
 
Nimewahi kwenda kagera wilaya ya kyerwa kuna sehemu panaitwa nkwenda....yani ulikua ukiingia kwenye kibanda umiza watu wote wanaongea kinyambo tu..nilikua nakwazika sana yani
 
Nilipo mimi kero ndogondogo hazikosi lakin ni kibanda umiza poa sana.
Kuna wakati unahisi uko london kabisa kumbe hapahapa kwa Juma Pondamali Mensah.
 
Kinachonikera mimi, watu wanajamba sana, kingine unakuta kuna sreen kama mbili au tatu. Kila mshabiki wa timu labda United au city kila m1 wanataka kuona timu yake. Wakati muda huo kuna game ya kufa mtu kati ya Rojiblanco na Barcelona.

Kingine mashabiki wengi wa aseno wananuka midomo maana hawaongei kwa muda mrefu sababu hawana furaha.

Mwisho kabisa kila tv imefunguliwa sauti tunasikia matangazo ya aina mbili tofauti.
 
Hahaha ananuka mdomo, bila shaka wa man u ananuka kwapa
 
Pole sana mkuu ndio kero yenyewe hiyo
Nimewahi kwenda kagera wilaya ya kyerwa kuna sehemu panaitwa nkwenda....yani ulikua ukiingia kwenye kibanda umiza watu wote wanaongea kinyambo tu..nilikua nakwazika sana yani
 
Ulikuwa masaki nn mkuu kwa vigogo
 
1. Linakuja limtu lireefu wewe umeshakaa na ka nafasi cha uangalia screen umejiwekea linakuziba kabisa

2. Linakuja lingine limevaa kofia linakaa mbele yako huoni tena

3. Lingine linakuja linavua shati kikwapa sasa

4. Linakuja lingine linapiga kelele mwanzo mwisho hata maneno ya mtangazaji husikii

5. Lingine linajifanya linaelekeza wachezaji namna ya kucheza kwa kunyoonya mikono utafikiri picha inamwelewa mwisho wa siku anakuwa anawaziba

6. Lingine linawasha sigara halafu eti linajifanya linapulizia mbali wakati upepo unazunguka mwishowe anawavutisha na wengine

7. Kuna wale wajasiriamali wa kuuza karanga au uji wanapita mbeleyako unakuta ndio kipindi muhuimu anakuziba
 
Ha ha ha u make ma day, kiufupi kibanda umiza ni kero, mi najipanga Tu niwe na tv langu nchi 53, na dstv naangalia hme na wife...aaah kibanda umiza hapana Kwa kweli mwishowe unaugua pumu hvi hvi
 
Dstv wameshusha bei funga kwako mkuu, hizi kero zinaboa sana
Hahahha. Home ni hny njoo ukae na mimi au hny nisaidie kuleta kitu chumbani au baba weka katuni au baba huku amekaa mbele ya macho yako .... ndo kero yenye raha yake. Ikiwa timu yako imeshinda, sasa ukifungwa na ni kipind cha kwanza hahahahah
 
Huku unakuta Man U ikifungwa goli watu wanaimba "Maguire kaliwa" au utasikia "Piga Magwaya haoooo!!". Kama ni mshabiki Wa Man U inabidi ubaki unatabasamu tu japo unaumia.
 
Kero kubwa ni Ushuzi.
 
[emoji3][emoji3][emoji3] yote kwa yote ndio raha ya bandani.
Kuna wengine mpira unaisha sauti imemkauka kuongea. Ukipigwa eti dakika ya 80 ukiinuka wanakuzuia hakuna kuondoka.[emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…