Kero tunazokutana nazo kwenye vibanda umiza

evonik

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2015
Posts
3,996
Reaction score
5,156
Heshima kwenu wakuu,

Awali ya yote tunamshukuru Mungu kwa kutupa nafasi ya kusonga mbele haswa pale tulipoona kipa anageuzwa tegemeo na wachezaji wote kumi. Mvinyo unapozidi kukaa ndipo unapozidi kuwa mtamu, kongole kwa Juma K. Juma. Kwa kuonesha umwamba na bado unaweza kuwa tegemeo kwa timu na taifa kwa ujumala.niende kwa mada

Kwenye vibanda umiza(vibanda vya kuangalizia mpira) kuna mambo mengi sana mengine yanafurahisha na mengine yanakarahisha.

Yanayokera ni pamoja na kelele nje yakibandaumiza,nilipokuwa-nangalizia kibanda umiza kimetenganishwa na ukuta unaotenganisha kibanda na garage ya magari, basi wale mafundi hupanda kwa juu kuangalia mpira coz juu pako wako wazi, mwenye kibanda umiza akiwa timua, basi wale mafundi wataenda kugonga machuma hata kama hawana kazi ili mradi tu watukere.

Pale ni kahama, nilipohamia pia kero zippo haziepukiki nakomaa nazo, hapa papya mwenye kibanda ni shabiki wa simba basi simba ikifungwa atakosa raha na hata mwishowe anakuwa hayupo active mfano simba ilipotolewa caf jamaa alikuwa hata kuwasha TV on time ni shida kwa mechi zilizofata.

Kingine ni wapo jamaa wana mtindo wa wakunywa soda nakubakiza nusu ndani ya chupa, kisha wanaitegesha kwenye bench, ukija kichwa kichwa ukiimwaga watakuganda uilipe.

Kingine ni wale back benchers, hawa wengi wao wanaingia huku wanasikiliza radio, goli halijaingia kwenye TV wao tayari wanashangilia, sometimes wanakera ila kama ni timu yako imeshinda utawapenda.

Na wewe tiririka kero ya kwako.
#KongoleTaifastaz#
 
Are you sure?
 
Kwani wenye vibanda umiza kauli yao ni ipi?

Sanchez magoli.
Hahaha nimecheka peke angu usiku huu uku porini.

Huo ndio utamu wenyewe wa vibanda umiza mtani. goli likiingia mmoja anachukua shati lake anaiziba TV ili msilione goli vizuri lilivoingia.

I miss you; ma uncle wazima wanaendeleaje.
 
Cha ajabu hao wa redio wakisema ni goli watu hata hawashangilii ngoja walione kwenye tv sasa ilo balaa lake kama una banda la mabati legelege jiandae kwa service kila siku.....
Kuingia na radio inaboa kinyama ,,goli bado halijaingia mfano penalt ndo inaenda kupigwa utasikia jamaa mwenye redio anasema ""amekosa"" uwa nataman nimpasue mtu kichwa [emoji3][emoji3]
 
Kibanda umiza cha hapa mtaan sijaona kero yake aisee hapa huwa Ni full mbilingembilinge za hatar humo ndani burudani safi sana
Projector 2
TV lg 3
game zote live.,, omba timu yako isiwe inapigiwa mpira utataman ukimbie humo ndan !! Nyimbo za hatar

Man u afe, afee [emoji2]

Aagh weekend huwa kunawaka moto mle ndan[emoji2][emoji2]
Missing those moments AF
 
Hahaha nimecheka peke angu usiku huu uku porini.
Hahahahaaa. Niliposikia kibanda umiza nikakumbuka kwenye ule uzi uliwahi kusema na wewe una kibanda umiza Mtani.
Huo ndio utamu wenyewe wa vibanda umiza mtani. goli likiingia mmoja anachukua shati lake anaiziba TV ili msilione goli vizuri lilivoingia.
Aiseee!!! Sijawahi ingia huko Mtani. Kumbe kuna mambo huko. Na si ajabu ukakuta ni mtu ambaye huwezi mdhania kama anaeza fanya hicho kitendo. 😀😀😀
I miss you; ma uncle wazima wanaendeleaje.
Nipo Mtani. Wote wazima kabisa Mtani.
 
Back
Top Bottom