Kero uwanja wa Benjamini W. Mkapa! Hali ni mbaya

Kero uwanja wa Benjamini W. Mkapa! Hali ni mbaya

Mtu mweusi NI KERO duniani

Anajua kusubiri kutengenezewa kitu kizuri yeye aharibu, hajui kutunza wala kurekebisha

Ni Waharibifu tu.
 
Kwanini ataje mkataba wa GSM kwenye suala la usafi wa uwanja ? Hii tabia ya makolo.
Huu uzi hujaletwa kiushabiki hapa, bila shaka utopolo wako umeshaingia kwenye sehemu yote ya ubongo wako!
Utopolo tabia zenu ni za kizwazwa sana, mnapoungana matahira kama wewe basi hata ishu yenue maslahi kwa taifa mnaleta ushabiki maandazi!
Ni vyema kwenye nyuzi kama hizi ukapita kimya kimya kama akili zako zimezubaa kama zako!
 
Kwanini ataje mkataba wa GSM kwenye suala la usafi wa uwanja ? Hii tabia ya makolo.

Kusikia gsm tu umeumia sana ama vipi?
Hata kama kama gsm inatajwa kama mfano ni kipi kinachokuuma? Haya kama unaumia GSM kutajwa kwenye huu uzi basi badilisha kila penye GSM weka MO ili uridhike Mr utopolo!
 
Wazungu si wachawi ila wanatumia akili kuishi, viwanja vyao katika kila mapato kuna % inayokwenda katika ukarabati na uboreshaji. Wasio wajibika wawajibishwe.
Hata kwa mkapa utaratibu huo upo, labda nikumbushie sakata la umeme kukatika wakati kila mechi kuna pesa inatengwa ya mafuta kumbe wanaitafuna matokeo meneja akafukuzwa. Wanachowaza watanzania wengi wanaopewa nafasi ni wizi mpaka caf au fifa watakapotufungia ndio wahusika wanashituka na kuchukua hatua
 
Tff na wizara ya michezo kwa ujumla pamoja na wahusika wengine wote akiwemo meneja wa uwanja, hili liwafikie!
Kiukweli uwanja wa Taifa unatia aibu sana, miundombinu imechakaa, viti vimechakaa vingine vimeng'oka, vingine vimepauka yaani kwenye majukwaa kwa kweli hali ni mbaya!
Uwanja huu ambao ulipewa jina la Benjamini Willium Mkapa ulizinduliwa mwaka 2007, na hadi hivi sasa ni takribani miaka 14 imekwisha pita na cha kushangaza viti vilivyowekwa tokea 2007 hadi leo hii ndio vilivyopo uwanjani!
Viti hivyo asilimia kubwa vimeshaisha muda wake ikilinganishwa na hali ya joto la Dar es salaam yaani vimeshalihimili jua hadi kiwango cha mwisho!
Kuhusu kwenye pitch wanajitahidi sana kukuza na kuzilinda nyasi ili majukwaani kwa kweli imezidi!
Haiingii akilini mtu analipa tiketi ya VIP lakini akifika kule anakuta kiti kinatobo katikati, au kimepasuka!
Hii ni aibu hata wageni wanaoingia pale huwa wanashangaa sana!
Mapato ambayo yamekwishaingizwa pale taifa ni makubwa sana na bado yanazidi kuingia, na vile vile serikali inatenga bajeti katika wizara ya michezo, isitoshe TFF inapokea fungu kutoka FIFA kwa ajili ya kuendeleza michezo ni kwa nini katika hayo mafungu kisitengwe kiasi kwa ajili ya kurekebisha miundombinu ya huo uwanja?
Hakika katika hili wadau na wapenda michezo yafaa kuhakikisha tunalisemea ili marekebisho yafanyike na uwe wa kisasa zaidi!

Zaidi pia miundombinu ya vyoo nayo haiko sawa, vyoo vingine vimeziba maji hakuna wakati mwingine yaani huko vyooni kunatia kichefuchefu!

Tff na serikali kwa ujumla msikazanie tu masuala ya mikataba ya gsm huko na clubs, tupieni macho pia kwenye huu uwanja mkubwa kabisa hapa Afrika mashariki ambao kwa sasa unaanza kuoza baadhi ya maeneo kabla haujaoza zaidi! Bado hamjachelewa...
Viti vingi vimeshavunjika na kupasuka.Juzi Kila kiti nikitaka kukaa nakutana na kiti kibovu,,,Ipo haja ya kufanya maboresho ya miundombinu siyo kukusanya tu hela
 
Back
Top Bottom