Kero ya Foleni Mbagala, viongozi mpo wapi?

Kero ya Foleni Mbagala, viongozi mpo wapi?

bestboy

Senior Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
181
Reaction score
172
Niende moja kwa moja katika hoja ya msingi. Leo nikiwa natokea maeneo ya kijichi majira ya saa mbili usiku, nimeshangaa sana kuchukua zaidi ya masaa mawili bila ya kufika mtongani. Yes naelewa ujenzi wa barabara unaoendelea lakini bado sitaki kuamini kwamba inaweza kuwa sababu ya kuwaweka watu njiani zaidi ya masaaa mawili kwa umbali wa kilomita zisizozidi 5.

Binafsi naona kuna uzembe mkubwa katika namna ya kumanage trafic na usimamizi wa hii miradi yetu kwa watu wanaopewa mamlaka hayo. Wako wapi viongozi wa wananchi wa Mbagala wanaoteseka na kero hii kubwa. Nimeshuhudia mamia ya watu wakitembea kwa miguu kuelekea mbagala kwa uzembe tu wa wasimamizi wa mradi na viongozi wetu.

Poleni sana wakazi wa Mbagala, nadhani tutaonana barabara itakapoisha.
 
Uliza watu wa Kimara, wakati barabara inajengwa kutokea Ubungo Mpaka Kimara. Kulala njia ilikuwa ni kawaida. Kucheleweshwa kwa masaa 3-4-5 hiyo ilikuwa ni kawaida, wala sio issue.

Nadhani wakati TANROAD wanajenga hizo barabara; angalau waweke utaratibu wa njia mbadala (Kama kuchonga njia mpya za pembeni); au waweke utaratibu wa kujenga upande mmoja mmoja; ili magari yaendelee kupita, hata kama kwa rate ndogo.
 
Back
Top Bottom