KERO ya Ku-block / Cease / Blacklist Matumizi ya NIDA NIN (National Identity Number); Tafadhali busara itumike tusirudishane zama za Kale,

KERO ya Ku-block / Cease / Blacklist Matumizi ya NIDA NIN (National Identity Number); Tafadhali busara itumike tusirudishane zama za Kale,

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
17,572
Reaction score
27,416
Ni kwamba huenda wewe yamekukumba hapo ulipo na wala haujui kama yamekukumba huenda unadhani upo salama kumbe haupo salama mpaka siku ukitaka service ambayo Taasisi itatakiwa kuvuta information zako NIDA ndio hapo utakutana na ujumbe wa THERE IS A PROBLEM PARSING MESSAGE RECEIVED FROM NIDA; au huenda ukawa kama huyu mdau aliyepata shida na kujibiwa majibu ambayo kama kawaida yetu nchi hii INA WAJUAJI WENGI WASIOJUA

Anyway kujua na wewe kama ni Muhanga unaweza ukajifanya unafungua Kampuni katika Brela na kujaribu kusajili akaunti

Je tatizo ni Nini ?
Kama nilivyosema awali wengi wetu hatujui na hilo ni tatizo la mamlaka husika kutokuwa warahisi wa kutoa maelezo / elimu; kama mdau hapo juu alivyouliza wadau na akaambulia kejeli, ila nimefanya my civic duty na kujaribu kuangalia huku na huku na nimekutana na habari moja ambayo lilitoka onyo kwamba wale ambao hawatachukua vitambulisho vyao ndani ya siku 30 (onyo lilitoka January) basi NIN zao zitakuwa blocked, Kama hivyo ndivyo kweli karne ya sasa ya Kidigitali tunalazimishana kufuata makaratasi ?, Na je kama kungekuwa na ulazima walishindwa kumtumia mtu SMS kwamba Kadi yako ipo sehemu fulani ?

Kero iliyopo
Watu ambao wamekuwa blocked wanakwenda NIDA wanajaza fomu (na kupoteza muda wao siku nzima) ili tu eti wawe unblocked baada ya masaa 24 (jambo ambalo najiuliza kwanini walikuwa blocked in the first place)? Hivi nguvu kazi zinazofanya blocking na unblocking kwanini zisingetumika hata kulima bustani ya nyanya huenda tungeongeza virutubisho mwilini na sio kutumia nishati (chakula), wino muda na makaratasi ya kujaza fomu ili tu kurekebisha jambo ambalo lilikuwa halina ulazima

Je kuna Ulazima wa Vitambulisho
Kwanini tunaingia gharama za bure kutengeneza haya mavitambulisho ambayo ya sasa kwa quality yake yanafutika baada ya masaa; kwanini kama information ipo isitumike hivyo hivyo online ? Kwanini tunaongezea watu mzigo na kazi sisizo tija kuwa block watu ? Eti wanasema sababu wanafanya hivyo ili watu wachukue vitambulisho?!!! Hii si ndio tunaita "To Cut your Nose to Spite your Face"

Kwa kumalizia namalizia na article ambayo inaelezea Tangazo la Kufutia watu NIN zao

Intent to cease use of NIN will hit govt more than individuals
Guardian 23rd January 2025

THE notice has been posted that individuals who are yet to collect their national identification cards have 30 days to do so at district offices, The National Identification Authority (NIDA) is getting weary on the situation, and had lately moved the cards from village and street or ward offices to district headquarters. The surprising aspect is that if they don’t turn up this will result in the suspension of using national identification numbers (NIN), now the sole element that the public desires.

It is unclear if there is no auxiliary legal empowerment or provision in law as to the use of the number, as different from holding the card itself, as the institution’s CEO was intimating. The idea that those who do not collect the cards would find themselves blocked from use of NIN, the key component of identification for essential public services, Not picking up one’s identity card in law can be called a tort, that is, an ordinary error, whereas freezing the NIN is potentially a breach of individual right.

Contrary to what the CEO stated that the NIN can be withdrawn at will, it isn’t the holder of NIN who would fail to use the number but NIDA would be blocking access to confirmation of that number by public institutions when the need arises. The idea that this blocking of access is punishment for not having picked up the card in which the number is embedded might not be really convincing for this or that public entity. They would resort either to other forms of identification or use earlier access to validate identity for that individual, that the lack of access isn’t their fault.

Explaining the move as intended to address the backlog of uncollected cards is valid only up to a point, as this is substantial to the issuing agency rather than the public, In that context, there is a risk for NIDA to lose its day to day relevance as most of those who need the number for mobile phone registration in particular already have them. They would be satisfied with the identity number they have, and don’t have to carry another card.

Surprisingly, looking at what President Samia Suluhu Hassan has been saying about national identification numbers, the fact that NIDA still has many such cards ought not to pose problems. What the president has been saying is less on the card as NIDA states but more on the numbers which people already hold, and the sort of improvements that the president was suggesting, are better on the numbers than on the cards. In other words, NIDA has an opportunity to build a databank with numbers, where cards will be made available if one really needs them, on request.

At that point all particulars relevant to an individual will have been updated, and even if no person seeks out cards, the agency could still keep an updated stock of information by means of interoperability of government information technology systems, what is known as e-government. When an individual registers anything, say a house, a matrimonial engagement or a bank loan, and there is a setting in which the name will click on systems that are interoperable with NIDA, or click something like an SMS on the name for NIDA attention, it will silently be updating those national identification numbers without ever issuing new cards.
 
Kwa nini watu wa NIDA wanakuwa na kiburi namna hii? Tumewaambia wasifunge hizo namba wenye namba wako hai watachukua tu vitambulisho vyao. Sasa wanapo block hizo namba halafu mtu anajitahidi kufika huko mbali alikojiandikisha anafika anakutana na madai mengine, mara ID, mara nini, inakuwa usumbufu, mtu anarudi alikotoka bila kitambulisho chake. NIDA fungulieni hizo namba wenye vitambulisho wanakuja kuchukua vitambulisho vyao. Kuna usumbufu wa kusajili laini na kurudisha namba za simu zilizopotea, mnataka watu wasajiliane laine za simu? Kama vipi anzisheni mchakato wa kujiandikisha upya watu wapate vitambulisho huko waliko
 
BRO Nakushauri FUATA ID KADI yako!

Kama uliweza kwenda kujisajili na wakakuuliza ujaze makazi yako ya kudumu UKAJAZA, Kitambulisho kimekamilika KWANINI HUENDI KUCHUKUA?

MAMLAKA zinapata majibu haya
1. Huendi kuchukua yamkini Umekufa
2. Huendi kuchukua yamkini haupo
3. Huendi kuchukua kwasababu umechonga feki mtaani unavimba na kadi feki.
4. Huendi kuchukua HUJUI UMHIMU

Sasa ili kuepusha yote hayo kujua upo na kurpusha udanganyifu nenda kachukue NIDA YAKO BRO!

KAMA HUENDI MAANA YAKE UMEKUFA Na sheria za NIDA ni kwamba kitambulisho kinaweza kufikia ukomo/ Expire kwasabu kuu mbili tu
1. Kufutwa kwasababu ya udanganyifu wa taarifa
2. Kifo cha mwenye nida.

UMESOMA VIZURI LAKINI HUTAKI KUFUATA CHETI CHAKO.... Na bado unataka utambulike kwenye maombi ya ajira bila cheti bro ebu kuwa serious bhana!

Kwenye hili vijana wenzangu tusiwe walalmishi sana kachukueni NIDA ZENU kabla serikali haijapitisha kanuni za kila raia kutembea na vitambulisho mtaani!
 
Tatizo hii nchi kila mtu anajiamulia...., hata wale tuliowapa dhamana ya kututetea inaonekana kama vile badala ya kututetea sisi wanatetea maslahi yao...

Badala ya kuwapima NIDA kwa kazi kama hii ya kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa identified wanawapima kwa kiasi cha GAWIO eti wanaowapa Serikali !!!!!!

BRO Nakushauri FUATA ID KADI yako!
Kwa fikra kama hizi no wonder wenye nchi hatupati Haki Yetu (Value for money) kwa kodi zetu kutokana na uelewa wetu finyu na kudhani kila zinachofanya Taasisi hizi ni Hisani na sio Kazi / Wajibu wao
Kama uliweza kwenda kujisajili na wakakuuliza ujaze makazi yako ya kudumu UKAJAZA, Kitambulisho kimekamilika KWANINI HUENDI KUCHUKUA?
Moja Makazi ya kudumu haimaanishi siwezi kuhama, pia unajua ni wangapi huwa wanakwenda kuchukua wanakuta havijafika ? Tatu nikiacha kuchukua hilo karatasi ndio mfute / block usajili wangu ? Tatu anayesumbuliwa hapa ni mimi pekee au Taasisi nyingi zinazoshindwa kutoa huduma / biashara sababu kila wakivuta details wanashindwa kupata hizo details ? Ukizingatia hizo Taasisi zinawalipa NIDA kwa kutumia Database ya NIDA
MAMLAKA zinapata majibu haya
1. Huendi kuchukua yamkini Umekufa
Kwamba nikichukua ndio sifi; na kama nikifa kwanini RITA isiwe connected na NIDA ili kuweka sawa Database
2. Huendi kuchukua yamkini haupo
Nikichukua ndio siwezi kutokuwepo ? Na nikiondoka kwani wanashindwa kuangalia Immigration ?
3. Huendi kuchukua kwasababu umechonga feki mtaani unavimba na kadi feki.
Feki maana yake nini ? Kwahio nikiwa na Fake Mtaani ndio wanifute kwenye Database ? Ukizingatia Kadi zenyewe hazina hata QR Code kwahio wangetaka kuzuia fake mtaani kwanini wasiweke QR Code ? Na kwa kuni block kwenye Database ndio mtaani nitashindwa kutengeneza Fake ?
4. Huendi kuchukua HUJUI UMHIMU
Kwahio wao ndio wananifundisha umuhimu ?
Sasa ili kuepusha yote hayo kujua upo na kurpusha udanganyifu nenda kachukue NIDA YAKO BRO!
Narudia tena ndio maana tukuwa short changed sababu ya mawazo kama haya...., HIO NIDA ni kwa kusaidia wenye nchi na TAASISI kujua kuna raia wangapi na information zao zipoje na SIO KUHAKIKISHA KILA MTU ANA KADI NYINGI KWENYE wallet au Pochi
KAMA HUENDI MAANA YAKE UMEKUFA Na sheria za NIDA ni kwamba kitambulisho kinaweza kufikia ukomo/ Expire kwasabu kuu mbili tu
1. Kufutwa kwasababu ya udanganyifu wa taarifa
2. Kifo cha mwenye nida.
KIFO Cha mwenye NIDA waunganishe na RITA ili kiweze kufutwa kuhusu undanganyifu kwanini walinipa in the first place kama nilidanganya ? Kwahio nikidanganya alafu nikakifuata nakuwa sijadanganya ?
UMESOMA VIZURI LAKINI HUTAKI KUFUATA CHETI CHAKO.... Na bado unataka utambulike kwenye maombi ya ajira bila cheti bro ebu kuwa serious bhana!
Kama ikifika wakati Vyeti vyote vikawa kwenye DATABASE basi kutakuwa hakuna haja ya Cheti Hardcopy, ndio maana leo watu BIMA wanakata online wala hakuna sababu ya kuhangaika na stickers; mwisho wa siku ni kurahisisha mambo na siyo kuya complicate
Kwenye hili vijana wenzangu tusiwe walalmishi sana kachukueni NIDA ZENU kabla serikali haijapitisha kanuni za kila raia kutembea na vitambulisho mtaani!
Narudia tena watu wenye mawazo kama yako no wonder tunaendelea kurudi nyuma....
 
Kwa fikra kama hizi no wonder wenye nchi hatupati Haki Yetu (Value for money) kwa kodi zetu kutokana na uelewa wetu finyu na kudhani kila zinachofanya Taasisi hizi ni Hisani na sio Kazi / Wajibu wao

Moja Makazi ya kudumu haimaanishi siwezi kuhama, pia unajua ni wangapi huwa wanakwenda kuchukua wanakuta havijafika ? Tatu nikiacha kuchukua hilo karatasi ndio mfute / block usajili wangu ? Tatu anayesumbuliwa hapa ni mimi pekee au Taasisi nyingi zinazoshindwa kutoa huduma / biashara sababu kila wakivuta details wanashindwa kupata hizo details ? Ukizingatia hizo Taasisi zinawalipa NIDA kwa kutumia Database ya NIDA

Kwamba nikichukua ndio sifi; na kama nikifa kwanini RITA isiwe connected na NIDA ili kuweka sawa Database

Nikichukua ndio siwezi kutokuwepo ? Na nikiondoka kwani wanashindwa kuangalia Immigration ?

Feki maana yake nini ? Kwahio nikiwa na Fake Mtaani ndio wanifute kwenye Database ? Ukizingatia Kadi zenyewe hazina hata QR Code kwahio wangetaka kuzuia fake mtaani kwanini wasiweke QR Code ? Na kwa kuni block kwenye Database ndio mtaani nitashindwa kutengeneza Fake ?

Kwahio wao ndio wananifundisha umuhimu ?

Narudia tena ndio maana tukuwa short changed sababu ya mawazo kama haya...., HIO NIDA ni kwa kusaidia wenye nchi na TAASISI kujua kuna raia wangapi na information zao zipoje na SIO KUHAKIKISHA KILA MTU ANA KADI NYINGI KWENYE wallet au Pochi

KIFO Cha mwenye NIDA waunganishe na RITA ili kiweze kufutwa kuhusu undanganyifu kwanini walinipa in the first place kama nilidanganya ? Kwahio nikidanganya alafu nikakifuata nakuwa sijadanganya ?

Kama ikifika wakati Vyeti vyote vikawa kwenye DATABASE basi kutakuwa hakuna haja ya Cheti Hardcopy, ndio maana leo watu BIMA wanakata online wala hakuna sababu ya kuhangaika na stickers; mwisho wa siku ni kurahisisha mambo na siyo kuya complicate

Narudia tena watu wenye mawazo kama yako no wonder tunaendelea kurudi nyuma....
UNA MAONI MAZURI lakini Serikali Hufanya mambo yao kwa bajeti na mipango;
Kwasasa UNATAKIWA UKACHUKUE NIDA YAKO KWANZA.

Hayo ya ku-link na mifumo kusomana siyo kazi ya kulala na kuamka siku moja bro ni mchakato wa kisera na kifedha.

Ingekuwa cheti cha shule ungeacha kukifuata kwasababu tayali umeshamaliza masomo?

Pole kwa changamoto lakini kwa maoni yangu ni bora unafuata kwanza nida yako halafu ukaendelea maoni kwa maboresho yajayo!

Tuseme na taasisi bila jaziba wanasikia na kuelewa kuliko tunavyodhania!

Sijui lakini yamkini uelewa wangu ni mdogo! Lakini nakushauri kachukue nida kaka!
 
UNA MAONI MAZURI lakini Serikali Hufanya mambo yao kwa bajeti na mipango;
Kwasasa UNATAKIWA UKACHUKUE NIDA YAKO KWANZA.
BAJETI na Mipango ?!!!!; Kumbuka hizo ni Kodi zetu na ufujaji wanaotumia kuchapisha vitambulisho ambavyo hata quality yake ni duni zingeweza kutumika kuongezea panadol mahospitalini au hata kumalizia miundombinu ya UMEME kuelekea Kaskazini ili tuache kutegemea kununua kutoka Nchi nyingine kama Ethiopia
Hayo ya ku-link na mifumo kusomana siyo kazi ya kulala na kuamka siku moja bro ni mchakato wa kisera na kifedha.
Kwahio ni rahisi ku block watu ambao tayari wameshaandikishwa ili tu mtu achukue kitambulisho chake ?!! ; Pili Taasisi mfano mitandao ya Simu ambayo inashindwa kufanya biashara kwa kupata wateja sababu tu wanashindwa kupata Data ya kama fulani mwenye hii Namba ndio yeye anayesema ni yeye ni nani anawalipa hizo hasara za kupata wateja potential ?!! Kumbuka hizi Taasisi zinawalipa NIDA
Ingekuwa cheti cha shule ungeacha kukifuata kwasababu tayali umeshamaliza masomo?
Nimekuuliza Cheti cha shule kipo mtandaoni ambapo Taasisi zote zinaweza kuniona ? Pili cheti cha shule kinahitajika pengi kama attachment NIDA sio hivyo NIDA inatumika kama identification katika mifumo mingi ndio Database MAMA ya Watanzania na Wakazi hivyo kuwanyima information hizo Watoa huduma ni kutokuwatendea Haki
Pole kwa changamoto lakini kwa maoni yangu ni bora unafuata kwanza nida yako halafu ukaendelea maoni kwa maboresho yajayo!
Nimekuuliza na ninakuuliza tena Nimekambia mimi nina Changamoto ? Kwahio wewe huwezi kusema jambo mpaka likukumbe..., hili jambo nilishaliona siku nyingi na humu kuna mtu alileta UZI ila matokeo yake ya Tanzania ya sasa yenye Wajuaji wengi wasio Wajuaji albakia kupewa kejeli badala ya msaada...

Tuseme na taasisi bila jaziba wanasikia na kuelewa kuliko tunavyodhania!
Wangekuwa wanaelewa wangesharekebisha hii issue sio ya leo wala jana huenda hata wewe umekuwa blacklisted lakini haujui sababu haujahitaji / Taasisi yoyote haijahitaji kuomba / kuvuta details zako kutoka NIDA
Sijui lakini yamkini uelewa wangu ni mdogo! Lakini nakushauri kachukue nida kaka!
Unaendelea kupita mulemule issue ingekuwa yangu au Kero yangu pekee wala nisingesumbuka kuanzisha UZI ningesolve personally ila hata wote ambao wamekuwa blocked leo wakienda ili wawe unblocked kama bado tatizo lipo palepale tutakuwa hatujatatua tatizo..., Tatizo linatatuliwa kwa kuondoa TATIZO Being reactive na sio proactive
 
Back
Top Bottom