KERO Kero ya maegesho ya malori makubwa katika eneo la makazi lililopo Folkland, Lumo, Vituka

KERO Kero ya maegesho ya malori makubwa katika eneo la makazi lililopo Folkland, Lumo, Vituka

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Naomba mamlaka husika zifuatilie na kujiridhisha kuhusu uhalali wa maegesho ya malori makubwa aina ya semi-trailer katika eneo la makazi lililopo Folkland, Lumo, Vituka, karibu na Nyumbani Lodge.

Malori haya yamekuwa kero kubwa kwa wakazi wa eneo hilo. Kutokana na uzito wake, unaokadiriwa kuzidi tani 10, kila yanapopita kwenye barabara ya mtaani husababisha mtikisiko unaofanana na tetemeko dogo la ardhi, kiasi kwamba hata watu waliopo ndani ya nyumba huhisi mtikisiko huo.

Aidha, malori haya yanachangia kuharibu barabara za mtaani ambazo hazikujengwa kuhimili uzito wa magari ya aina hiyo. Vilevile, yanaporudi kuegeshwa, husababisha kelele nyingi kutokana na eneo kuwa finyu, hali inayowalazimu madereva kutumia muda mrefu wakielekezana namna ya kuyaingiza na kuyaegesha.

Soma Pia: Malori yanayopaki eneo la urafiki ni kero kwa watumiaji wa Barbara ya morogoro

Tunaziomba mamlaka husika kuchunguza iwapo maegesho ya malori makubwa katika maeneo ya makazi yanafuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa. Ikiwa kuna ukiukwaji wa taratibu, hatua stahiki zichukuliwe ili kulinda usalama, utulivu na miundombinu ya wakazi wa eneo hilo.
 
Back
Top Bottom