A
Anonymous
Guest
Mke wangu amekuwa akihudhuria kliniki ya ujauzito katika Kituo cha Afya Kinyerezi. Kila anapokwenda kwa ajili ya huduma za kliniki, amekuwa akitozwa Shilingi 6,000 bila kupewa maelezo ya wazi kuhusu sababu ya malipo hayo.
Pia, anapougua huendelea kutozwa fedha za kumuona daktari pamoja na gharama za dawa, hali ambayo inaonekana kwenda kinyume na utaratibu wa kutoa huduma kwa wajawazito.
Tunaomba mamlaka husika zifuatilie suala hili na kutoa ufafanuzi kuhusu uhalali wa malipo hayo, pamoja na kuhakikisha wajawazito wanapata huduma stahiki kwa mujibu wa sera na miongozo ya afya.