Kero ya taka Mijini, kila Mtaa wamiliki "incenerator"

Kero ya taka Mijini, kila Mtaa wamiliki "incenerator"

May Day

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Posts
6,311
Reaction score
9,027
Incenerator ni Mtambo utumikao kuteketeza taka. Mitambo ya aina hii ni maarufu sana kutumika kwenye Mahospitali na Viwandani, ila pia ipo Mitambo mikubwa na midogo kwa ajili ya kutumika majumbani.

Ukizunguka kwenye Miji hii mikubwa kama Jiji la Dare Es Salaam, Arusha n.k lazima utakubaliana na mimi kuhusu hili, ukikatiza kwenye mitaa utakutana na Viroba vya taka vilivyorundikana, nimezunguka maeneo ya Mbezi hali ya taka ni mbaya na sina shaka hali ipo hivyohivyo kwenye maeneo mengine.

Kwenye Mitaa tunaweza kuchangishana au kumpa Mtu au Kikundi cha Watu tenda ya kuendesha Incenerators hizi ili kuondokana na kero ya kuzagaa kwa taka kwenye mitaa.

Wakazi wa Mtaani wataendelea kuchangia kwa gharama nafuu tena kwa ubebaji rahisi kwani hakutahitajika rasilimali za gharama ya juu kutoa taka kwenye Nyumba zao na kuzifikisha kwenye Incenerator. Vijana wanaweza kukusanya tu taka hizi kwa kubeba, kwa Toroli au kwa Guta kwani zinaenda umbali mdogo tu.

Na baada ya kuteketeza taka zinazohitaji kuteketezwa yale mabaki ya vyakula, matunda na mboga yazalishwe Mbolea ya Mboji.

Kuna ukusanyaji wa chupa za plastiki Mitaani, lakini ukusanyaji huu unabagua aina fulani ya chupa, kwa nini Mamlaka zisikubaliane na hawa Wadau ili Waokotaji wakusanye chupa zote wao waende wakazitenganishe huko vituoni kwao? Hii itasaidia kuziondoa plastiki zote mtaani na baadae kutafuta kwa kuzipeleka zile zisizohitajika/faa kwa urejeshaji.

Na ikifaa zaidi Waokotaji waanze kukusanya pia hata nailoni na pakiti za Plastiki nazo zikatenganishwe huko huko.

Huenda tukadhani tunakwepa gharama za kudhibiti hizi taka za plastiki lakini huko mbele bado ikatugharimu mara milioni moja.
 
Wazo zuri.
Miji imeelemewa na wingi wa taka kila kona.

Cha kustaajabisha hizi taka ni malighafi...Mamlaka ziwezeshe/zitengeneze Wajasiriamali wa kurjesha taka.

Kuwe na eneo kwenye kila Kata au Tarafa ambako kutakuwa na miundombinu ya kuwezesha kupokea taka na kutenganishwa,...Wajasiriamali wazalishe mbolea, vyakula vya mifugo n.k kutoka mabaki ya vyakula na matunda..

Hii itafanya ukusanyaji wa taka ukawa jambo la kuvutia Waokotaji/Wajasiriamali kama inavyofanyika kwa taka za plastiki.
 
Serikali hasa hasa Serikali za Mitaa ndo tatizo Tanzania.
Wao ndo wameruhusu ujenzi holela sababu ya rushwa

Wao ndo hawafatilii waokota uchafu

Wao ndo wameshindwa pangilia mitaa vizuri
 
Back
Top Bottom