KERO Kero ya vyama vya wafanyakazi hasa TALGWU (chama cha wafanyakazi wa serekali za mitaa) kutengeneza Tshirt mbovu za wanachama wao

KERO Kero ya vyama vya wafanyakazi hasa TALGWU (chama cha wafanyakazi wa serekali za mitaa) kutengeneza Tshirt mbovu za wanachama wao

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Syv

New Member
Joined
Jan 1, 2023
Posts
3
Reaction score
2
Kila mwaka vyama vya wafanyakazi vinasherekea siku ya wafanyakazi yaani mei mosi na sherehe hizi zinaendana na kutengeneza sure hususan Tshirt au kutoa khanga kwa ajili ya kushona.

Jambo la kusikitisha licha ya kuwakata wafanyakazi ambao ni member wa vyama hivyo Kila mwezi kwenye mishahara yao mfano wafanyakazi wa serekali za mitaa TALGWU kila mwezi wanakatwa pesa LAKINI siku za mei mosi watumishi wanaambulia Tshirt au khanga mbaya na zisizokuwa na ubora wa kueleweka hii ni sawa na utapeli hivyo viongoz wa vyama hivi vya wafanyakazi wajitathimini kimsingi hatufurahishwi na jambo hilo.

Hoja hii pia inaenda moja kwa moja na vyama vya kitaaluma kama chama cha usajili wa wahandisi ERB ambao wanachama kila mwaka wanalipia pesa zaidi ya 400k kuhudhuria tu mkutano mkuu wa mwaka LAKINI pia tunapewa tshirt zenye ubora mdogo na zisizo vutia pamoja na mabegi feki ya kichina ambayo ki kubwa yana nembo ya ERB jamani hata kama ndo kupiga members wenu sio kwa staili hiyo hivyo viongoz wa ERB pia wajitathimini kwa hilo kwani mtu baada ya kumaliza mkutano mkuu kikubwa hizi Tshirt huwa tunafanya dekio na mabegi tunawapa msaada watoto wa shule za msingi wenye uhitaji hazifai.
 
Sijawahi ona umuhimu wa hivi vyama zaidi ya kukata pesa za watumishi at least watoe Tshirt au hizo kangha za ubora wa kueleweka kwa members wake hiyo once per year. Kuliko kuvalisgana midosho
 
Back
Top Bottom