kero yangu kwa baadhi ya dada zangu

shabani ally

New Member
Joined
Nov 14, 2011
Posts
1
Reaction score
1
leo itabidi niwaseme kupitia nafasi hii,jamani kuna baadhi ya wanawake wanatakiwa wajitambua thamani ya utu wao na miili yao,nasema hayo kutokana na research yangu isiyo rasmi.Kuna akina dada wanajichubua hadi wanajiharibu kabisa thamani ya miili yao,yaani utakuta mtu usoni mweupe sana lakini kwenye mikono na miguu huwa weusi sana,sasa sijafahamu kwamba tatizo ni kwamba vioo vyao huwa ni vya kujiona sura tu au dawa wanazotumia sio mzuri,lakini kwa kawaida mwanamke anaye jitambua huwa anapaka lotion ambayo inamfanya tu kuwa na soft skin na sio kumbadilisha rangi ya ngozi yake.jamani dada zangu kuweni makini na swala hili kwa kuwa kuna rafiki yangu sikumoja alinitamkia huwenda akamuacha gf wake kisa mkorogo anao utumia unatoa harufu mbaya hali ambaye humpa karaha wakati wa kukutana,na pia anajisikia vibaya kumtambulisha kwa marafiki zake ambao anahisi wana uelewa kidogo kwa kuwa ana ogopa kudharauliwa."jitambueni bwana"
 
Asante kwa kutukumbusha, tutatafuta dawa ambazo hazina hizo side effect ...
 
Maisha ni yao. Miili ni yao.

Kama wale wanaoshonewa manyewele bandia wana haki ya kufanya hivyo basi na wanaotumia mkorogo wana haki zote za kujimenya.

My philosophy is live and let live.
 
wanaume wa siku hz baadhi yao wanajichubua. Sasa cjugq utasemaje
 
sasa kama dada zako wanajichubua ni malezi ya familia yenu
ukiachia mbali hao dada zako kuna hata wanamme wanajichubua, angalia waigizaji wa kiume wa ta na baadhi ya waimbaji
tena wameenda mbali hadi wanaweka zazuu

Usituchoshe, hutulipi hatukulipi
 
Siku hizi wote twafanana wanawake, wanaume wote wanajipiga mkorogo, wanasuka, wanapaka mapowder, wanja na lipstick! Ushauri ende na kwenu pia.
 
Ray na Kanumba ni wazee wa mkorogo. nashangaa sana janaume zima linashindwa kumuangalia mtu kama Akon anavyoshine kwa rangi yake halisi!!
 

Umefulia kasuuze na maji ya bomba!!! Muangalie Nyoshi, wale kina poyoyo a.k.a masharobaro. Angalia wanabongomovies na wanamuziki utaona mambo!!! Pale manyanya kuna viME huwa vinajianika hapo........ngozi kama kitifire alafu vimejipodooaaaa kama vikatuni!! Shutuuu..........mwaona wanawake tu nyie.....ebo!!!
 
Waambie bana! wamezowea! kuna mmoja hapa kazini ana maskio meusi lakini uso rangi ya maria carey.
 
Unakuta mwanamme anaudharaulisha uanamme wake kwa tsh 2134

ana mkorogo karolait 552, ana dred za 250, ana mihereni, licheni kubwa kama nyororo, bracelet kubwa, na lipete kama embe vyooote alinunua kwa mafungu 400

Na ivi wameifuma ile ya kusokotesha vinywele kama mkutano wa nzi, vijana wanafanya maonesho kwakweli!!
 
Na ivi wameifuma ile ya kusokotesha vinywele kama mkutano wa nzi, vijana wanafanya maonesho kwakweli!!

nyepesi nyepesi ni kwamba huku mpwapwa wanaume ndio wanaongoza kwa kujichubua.
 
Ila ukienda Tanga ndiyo utashangaa zaidi wanawake ni weupe kwa asili lakini bado wanajichubua hadi wanakuwa wekundu na mishipa ya damu inaonekana sasa sijui wanatafuta rangi gani nyingine. Wanaume wanaopenda kujichubua naona wengi wao ni wa-congomani ndiyo wanaambukiza wabongo.
 
Kujichubua wajichubue wengine kukereka mkereke nyie. Waja bana!
 

tanga sehemu gani nikashuhudie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…