shabani ally
New Member
- Nov 14, 2011
- 1
- 1
leo itabidi niwaseme kupitia nafasi hii,jamani kuna baadhi ya wanawake wanatakiwa wajitambua thamani ya utu wao na miili yao,nasema hayo kutokana na research yangu isiyo rasmi.Kuna akina dada wanajichubua hadi wanajiharibu kabisa thamani ya miili yao,yaani utakuta mtu usoni mweupe sana lakini kwenye mikono na miguu huwa weusi sana,sasa sijafahamu kwamba tatizo ni kwamba vioo vyao huwa ni vya kujiona sura tu au dawa wanazotumia sio mzuri,lakini kwa kawaida mwanamke anaye jitambua huwa anapaka lotion ambayo inamfanya tu kuwa na soft skin na sio kumbadilisha rangi ya ngozi yake.jamani dada zangu kuweni makini na swala hili kwa kuwa kuna rafiki yangu sikumoja alinitamkia huwenda akamuacha gf wake kisa mkorogo anao utumia unatoa harufu mbaya hali ambaye humpa karaha wakati wa kukutana,na pia anajisikia vibaya kumtambulisha kwa marafiki zake ambao anahisi wana uelewa kidogo kwa kuwa ana ogopa kudharauliwa."jitambueni bwana"