Kero za Cinema

Kero za Cinema

Satirical Yet Awesome

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2023
Posts
629
Reaction score
1,688
Kwema wakuu

Aisee jana nilienda kuangalia movie mida ya usiku, nilikaa mbele ya mdada flani ivi ambaye mwanzoni nilidhani atakuwa mtaratibu tuu kwasababu alivofika alianza kusalimia watu wote wa karibu yake ila kilichofata nilitamani nihame.

Yaan huyu mdada kwanza anapiga makelele, kitu cha kushtusha kikitokea kweny movie anapiga makelele hadi theater nzima inashtuka watu wanaanza kumwangalia, kikitokea kitu cha kuchekesha anacheka kwa nguvu kuzidi kila mtu.

Mi napenda sana utulivu wakati naangalia movie, ndio sikatai kuna yale makelele ya pamoja au kuna ile watu wanapiga makofi when something good happens, hayo hayana shida but shida ni kwamba ni yeye tuu ndo anapiga makelele alaf niko mbele yake.

Movie ikiwa inaendelea utasikia anaongea kwa nguvu "ooh that's good" "I like that" "Told you bitch" "what the f*ck" hadi watu wa mbele wakawa wanageukia kuchungulia nani anafanya hivo, hapo bado aliponikera zaidi kuna muda akiongea sana anaanza kunipumulia mara apige miayo na kwa kuwa hajaegemea siti, ile pumzi yake inakuja hadi kwangu naanza kusikia harufu za popcorn alizokuwa anakula, aisee ni SHIDA, siku enjoy kabisa hadi movie inaisha.

Sijui alikuwa anatafuta attention au anajaribu kufurahisha watu ila alichofanikiwa kufanya ni kukera watu especially me.

Siku nyingine niliyokereka ilikuwa mwaka huuhuu but miezi ya mwanzoni, nilikaa row moja na madogo flani wawili wakike na wakiume, walionekana kama wapenzi na walikuwa wanapigo flani ivi kama wanachuo, mwanzoni kila mtu alikaa kiti chake wakati movie inaanza, badae nikaona wanapakatana, badae kidogo naanza kuona wanaanza kushikana wakijichekesha, badae tena wanaanza kupigana mabusu huku sasa wanashikana serious mara wanashikana matiti mara jamaa aingize mkono wake kweny suruali ya demu, aisee I know it's not my business kufatilia wanachofanya but public places kama cinema sio sehemu za kufanya hayo mambo, mi nikawaacha nikaendelea zangu kuangalia movie.

Huu ndio ushuhuda wangu kwa leo, tujaribu kuwa wastaarabu tunapokuwa kweny public places.
 
Back
Top Bottom