KERO Kero za Huduma Hospitali ya Misungwi Wilaya Misungwi Mkoa Mwanza

KERO Kero za Huduma Hospitali ya Misungwi Wilaya Misungwi Mkoa Mwanza

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Huduma katika hopstali hii ni mbaya sana ingawa hosptali ina majengo mazuri ya kisasa vifaa vya kisasa, lakini kila tukienda Wanasema mtandao hakuna.

Na pia Serikali iweke wazi kama haiwalipi mishahara wauguzi tujue ili sisi wenye wagonjwa tulipe pesa zetu maana nilipeleka mgojwa mpaka masaa 24 hajapata huduma wala vipimo sababu ni mtandao na 4,000 ya kufungua file.

Kiufupi wauguzi ni wazito sana, hawatoi huduma kwa weledi mpaka uwasukume kwa chochote au uwe na unayemfahamu.

Serikali ituweke wazi sisi tunaopeleka ndugu zetu kama hawalipwi mishahara basi tulipe sisi wenye shida. Muuguzi anaacha wagonjwa mapokezi anaenda kunywa chai na hakuna anaempokea.

Kwanini Misungwi mnatufanyia hivi?
 
kama kipato kinaruhusu mgonjwa wako mpeleke private tu....... .

Scenario kama hizo ni nyingi sana. ..pole
 
Hiyo hospital kuna siku mtu aliandikiwa vipimo vya full blood picture kwenye karatasi kwa mwandiko wa mkono.
 
Back
Top Bottom