Kero za mahotelini na migahawani

milionea wa kesho

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2015
Posts
328
Reaction score
631
sio kila mara unakula nyumbani. mara nyingine unalazimika kwenda kula migahawani au mahoteli. Ni experience gan mbaya ushakutana nayo? weka kero yako hapa.

as for me, kuna siku nimeenda kula kwa mamantilie mmoja hivi maeneo ya sabasaba Dodoma. kuna mhudumu mmoja mzuri kama malaika ana rangi ya kahawia na alikuwa na msambwanda mkubwa sana na alivaa suruali iliyomkaa vema.

wakati ananihudumia nilipigwa na harufu kali ya jasho la kwapani hadi hamu ya kula ikaisha. nikatoka nduki sikurudi tena.


share ur experience
 
Kuna siku nilikuwa na njaa kali nikapita mgahawani nipate msosi. Sahani zikaadimika, nikaona niwahimize waliokwenda kuandaa Sahani hizo.

Nilipofika wanapozisafishia nikayaona yale maji waliyokuwa wanasafishia , nilirudi mbio nikapitiliza mkate na soda kwanza ili kupunguza stress
 
Bado sijafika level za kula hotel so kwangu ni mgahawan na mama ntilie lakin kote huko sijawahi kuvumilia kutumia vyombo vya plastic au bati kwa kulia chakula au kunywea chai/maji.

Kwa kifupi vyombo vya plastic na masahan yale ya bati yenye partition huwez kuniwekea chakula nikala.Siwez hata siku moja bora nikae na njaa yangu.

Ishu nyingine ni kwamba huwe najiskia kichefu chef kabisa kula mchuzi au mboga iliyoungwa na nyanya halaf nyanya hizo zikashindwa ku dissolve kwenye harakat za kukaanga mboga.Nikiiona nyanya (vipande) ambavyo vinaonekana waz waz kwenye mchuzi aaah hapo kwangu bonge la mtihan.

Kwa kifupi nina maeneo maalum ya kula sio kila sehem naweza kula kwa kuzingatia vigezo /changamoto tajwa hapo juu

Nawasilisha
 
mkuu upo kama mm.
nikionaga sahani za plastiki najisikia kichefuchefu.

na hayo manyanya yakiwa hayajaiva ndo sigusi kabisa bora nile wali mkavu
 
tatizo wanakuwa na haraka kuwahi wateja
 
Labda alitoka kununua mkaa mtaa wa jirani.
 
hua nakereka nikienda migahawani muhudumu aniulize nachokula then asilete aje aniulize tena eti kasahau
na kuna wale unamuagiza afu haleti anaenda kuhudumia wengine
bila kusahau kwa mama ntilie anapokea pesa huku anasukuma chapati
 
Niliwahi kwenda hoteli moja hapa dar, wahudumu na wapishi ni wanaume wanaovuga mafurushi ya madevu, mboga ilikuwa na vipande vya nywele sikula kile chakula nililipa na kusepa
 
ukienda kula kwenye migahawa usiangalie sehemu hizi - wanaoshea wapi vyombo vyao, maji wanayotumia ynafananaje.

pia usiende jikoni kuona wanapikaje(jasho, wanajifutaje mikono, etc)

pia sehemu mnaponawia mikono usimwangalie aliyekutangulia kanawaje au ananawaje maana vyote hivyo ni majanga.

kula nyumbani upate mlo ulioandaliwa kwenye mazingira salama.
 
U
Usinikate stimu mkuu, nimekaribia kwenda gengeni hapa
Usikatike stim mkuu kale TU,mi nilikuta kifungu cha nywele ktika wali sijui zilikuwa za juu Kati au chini njaa ikantumbukia nyongo
 
mifuko ya plastic ndiyo hotpot ya kutunza joto, madhara yake ni makubwa mno hasa kwenye magonjwa ya kansa. nashukuru serikali kupiga marufuku matumizi ya mifuko hii
 
Mimi sijawahi kufikiria swala la usafi kwenye migahawa, ndiyo maana kila siku sehemu yangu ya kula ni pale kwa mama ntilie wa mabanda ya bati ya Mshikamano, mitaa ya soko kuu la Majengo Dodoma.
 
Kuna mgahawa niligoma kutumia vyombo vya plastic na bati. Ikawa wakiniona nimeingia...wanatafuta vyombo na kunitengea.
 
mifuko ya plastic ndiyo hotpot ya kutunza joto, madhara yake ni makubwa mno hasa kwenye magonjwa ya kansa. nashukuru serikali kupiga marufuku matumizi ya mifuko hii
Mi nashukuru kwa kuwa nimepata chanzo kingine cha pesa
 
Mi nashukuru kwa kuwa nimepata chanzo kingine cha pesa
Jana nimefika kwa mama ntilie anauza supu alikuwa amekata nyama mapande makubwa ukihitaji ya kiasi chochote cha fedha kuanzia elfu anakukatia basi nikaomba ya 2k si akaanza kuchagua into nzuri kwa mikono haa! Nilimwambie nitakula mishikaki aache tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…