Kero za TRA Kinondoni (Mwenge)

connections

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2013
Posts
2,190
Reaction score
3,039
Wadau natumaini wazima yapata mwaka sasa toka nianzishe biashara yangu ya MINI SUPERMARKET sasa nikaona ngoja nifanye kihalali nikaenda TRA so nkatakiwa kulipia kodi ya MAPATO duuh sasa huo usumbufu wa kulipia kodi pale MWENGE (Mkoa wa ki-Kodi wa KINONDONI) unanifanya nifikirie kukwepa kodi maana kwanza huo mlolongo wa mpaka kulipa kodi na majibu mabovu ya staff wa TRA unanichosha yaani mtu unawapelekea pesa bila kulazimishwa lakini mpaka unajuta fikiria unafika unajaza fomu, unapanga mstari kuelekea dirishani ati kupigiwa muhuri kisha uelekee benki (NMB) nako mzinga wa foleni kisha urudi tena TRA zinga la Foleni tena in short unahitaji siku nzima.

SASA kupata ROAD LICENCE unafuata utaratibu wa kwenda mapokez uchukue fomu, zen dirishani kuandikiwa kiasi cha kulipia zen uende benki urudi tena kwenye foleni ya kuelekea dirishani TRA ukifika unaambiwa uje baada ya SIKU 3. Duuuh! Mimi nililipia tar 13/05/2013 nikaambiwa nije Alhamisi 16/05/2013 kurudi nikaambiwa Road Licence bado niende Ijumaa 17/05 nikaambiwa bado nije j3 (20/05) nikaenda nikaambiwa niende Alhamisi 23/05/2013 duuh kweli namna hii watu watakuwa motivated kulipia kodi au mnatufundisha kukwepa kodi?
 
Pole kaka hii ndio Tanzania,ila nazano unaweza kulipa kodi kupitia postalbank siyo lazima kwenda TRA
 
wapuuzi wale mm nilikua nataka VRN majibu waliyonipa kwa kweli nimeacha na naendelea na biashara bila kulipa VAT
 
Hivi Ndugu Connections bado unajipeleka TRA kulipa kodi mwenyewe hapa TZ? mimi binafsi nilianzisha biashara ya DUKA la MATAIRI ya Magari pale KARIAKOO nikawa naenda kulipa KODI TRA ILALA siku moja nilikaa foleni toka saa 3 asubuhi mpaka saa 8 mchana halafu nikaenda benki nikakuta foleni (wanaolipa kodi na wateja wa kawaida wa benki) kurudi TRA saa 11 kasoro jioni. kuanzia siku hiyo niliapa silipi kodi nitatafuta risiti feki kwa vishoka mtaani mambo yanaenda. TZ ukijidai mzalendo wa kulipa kodi zote utakuwa unawafanyia kazi TRA na viongozi wanaotumia kodi zetu kwenda Ulaya, Afrika Kusini na India kutibiwa Mafua na kupima uzito. Wakati hospitali hazina madawa, mashuleni hakuna madawati, Mwl. mwenye shahada ya kwanza (Bachelor Degree) kule kijini anaefundisha watoto/wadogo zetu kule kijini analipwa mshahara mdogo kuliko mfagizi wa ofisi ya TRA. KAMA NOMA NA IWE NOMA. WAMEMWAGA UGALI MI NAMWAGA UGALI TUONE NANI ZAIDI.
 
Wana hasira wale wafanyakazi. Baada ya kuanzishwa kwa utaratibu wa kulipia benki siku hizi hawakati noti kabisa, wao kazi yao imebaki kucheza na makaratasi tu
 
kivipi? Hebu nifafanulie hapo

Sina uzoefu na hili swala ila nilisikia kama tayari una Tin number na unajua kiwango chako cha kodi unacho lipia unaweza kwenda postalbank ukalipia huduma zifatazo. New driving license fee,income tax,development levy,property tax na custom tax. Na ukiangalia kwenye webside ya postalbank wameandika ni kweli wanatoa hizo huduma ni vizuri ukaenda watakupa utaratibu.
 
Wana hasira wale wafanyakazi. Baada ya kuanzishwa kwa utaratibu wa kulipia benki siku hizi hawakati noti kabisa, wao kazi yao imebaki kucheza na makaratasi tu

sipati picha siku tanesco nao wakianzisha utaratibu wa kulipia bank, nahisi itakuwa full minuno hapo ofisini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…