Kero ziletwazo na wateja wasumbufu kwenye biashara

Kero ziletwazo na wateja wasumbufu kwenye biashara

kinywanyuku

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2015
Posts
3,746
Reaction score
2,924
wakuu habari zenu mimi mfanyabiashara wa viatu vya kike tatizo lilionitokea hili mteja alikopa viatu vya elfu kumi tano akalipa akabakiza elfu mbili sasa akaja tena dukani akaomba kukopa mkoba elfu kumi sasa vile viatu imepita wiki tatu kavaa vikambandukia sorry kakataa kumaliza deni la mkoba je ni halali wakuu isitoshe me viatu nilichukua kkoo kwa dazani sikujua ubora wake maana me nilchagua vizuri ili kuwavutia wateja sasa nimfanyaje huyu mteja wadau maana naona kanikata faida
 
Badili tactics zako za biashara.

Especially hapo pa kukopesha.

Manake kuna wanawake mnnnnnh.
 
Kazi ipo hapa. Hata nashindwa kukushauri ufanyeje. Badili tu namna unavyofanya biashara yako.

Sikushauri kukopesha.
nashkuru mkuu yaani nimekaa naumiza kichwa mtu nimemkopa viatu kavaa wiki tatu halafu vimechanika aje kunikomoa kwenye bidhaa nyingine
 
Mtu akileta mada huku ni wazi kuwa amejaribu sana na Ameshindwa so anakuja huku kupata mawazo tofauti. Nashangaa mambo madogo ambayo unaweza uka-deal nayo bila hata mkeo kujua(kama unae)

Samahani sana kama nimetumia lugha ya makwazo
 
nashukuru mkuu nafikiri nitabadilika sasa maana nilikuwa nawakopesha sana wanawake huyo ndio kaniharibia kabisa anataka asilipe deni la bidhaa nyingine kisa viatu aliviharibu
Tujifunze kuwa mkopo kwa bidhaa ambayo haina warrant ni hasara kwako

Na kumkopesha mtu bidhaa ambazo hazina ulazima ni kujitengenezea mfereji wa kufirisika
 
Mtu akileta mada huku ni wazi kuwa amejaribu sana na Ameshindwa so anakuja huku kupata mawazo tofauti. Nashangaa mambo madogo ambayo unaweza uka-deal nayo bila hata mkeo kujua(kama unae)

Samahani sana kama nimetumia lugha ya makwazo
ndiyo hivyo mkuu nilitaka waliopitia changamoto kama yangu walifanyaje,walimnyang'anya mteja bidhaa au walihesabu kama hasara wakapotezea
 
Tujifunze kuwa mkopo kwa bidhaa ambayo haina warrant ni hasara kwako

Na kumkopesha mtu bidhaa ambazo hazina ulazima ni kujitengenezea mfereji wa kufirisika
nashkuru sitafanya ujinga huu tena maana nilizoea kuwakopesha wafanyabiashara wadogo kila siku wanipe buku
 
Hata sisi waunza majeneza na vumbi la Kongo pia tunakutana na changamoto!
eeh mteja akileta kama hizo alizonipiga mimi unaanzisha ugomvi au unamkaushia tu nakuhesabu hasara tayari
 
Back
Top Bottom